Na Mwandishi Wetu
Shule ya Sekondari kichangachui iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji imenufaika na ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango anayoendelea nayo Mkoani Kigoma kwa kupata Kompyuta kumi (10) kwa lengo la kufundishia na Kujifunzia.
Kiongozi huyo alitoa ahadi ya kutoa kompyuta kumi (10) Jana July 09, 2024 Wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari hiyo wakati wa kukagua eneo linalojegwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi na Chuo kikuu cha afya na Sayansi Shirikishi cha Mhimbili (MUHAS) kampasi ya Kigoma.
Makamu wa Rais alimtaka Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Ngenda Kilumbe kukabidhi Kompyuta kumi na mbili (12) alizoahidi na ambazo tayari zimeshanunuliwa.
Aidha alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Maji kwa lengo la kuchimba kisima cha Maji ili kuongeza uwepo maji mda wote katika Shule hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba alisema kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali itaajiri Walimu elfu kumi na Mbili (12, 000) huku akimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kufanya msawazo wa Walimu kwa Shule zenye upungufu .
Kupatikana kwa Kompyuta kumi (10) za Makamu wa Rais, Kompyuta kumi na mbili (12) ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kunafanya Shule hiyo kuwa na jumla ya Kompyuta thelathini na Mbili (32) za kufundishia na kujifunzia.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa