Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji amewataka Watumishi ambao ni ajira mpya kufanya kazi kwa weredi kwa kuzingatia Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Ameyasema hayo Leo March 07, 2025 alipokuwa akifunga mafunzo kwa Watumishi hao ambao ni ajira mpya katika kada ya Watendaji wa Mtaa, Elimu Sekondari na Afya.
Amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni eneo salama katika Utumishi wa Umma huku akiwataka kila mmoja kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuishi kulingana na tamaduni za eneo husika.
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea Wataalamu ajira mpya 112, Watendaji wa Mtaa wakiwa 10 Walimu Elimu Sekondari 35 na Wataalamu wa afya 67.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa