Na Mwandishi wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeibuka mshindi wa pili huku Halmshauri ya Wilaya ya Uvinza ikiibuka mshindi wa kwanza kwa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma katika sherehe za maonesho ya Wakulima nane nane yalihofanyika kikanda Mkoani Tabora Manispaa ya Tabora katika Viwanja vya Fatuma Mwasa yaliyofungwa
Yakifungwa hapo jana na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenya Mkoani Tabora Halmashauri, Kampuni , vituo vya Utafiti vya mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Taasisi za Umma zilisomwa kutokana na ushindi na nafasi katika kushiriki kwao, bidhaa na mazao ya Kilimo na Mifugo yaliyooneshwa
Katika Ushindi huo Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo iliibuka mshindi wa tatu katika Halmashauri za Mkoani Kigoma huku Halmashauri ya Urambo ikiibuka mshindi wa kwanza kwa kwa taasisi zote zilizoshiriki huku ikishikiria nafasi ya Kwanza kwa Halmashauri zilizopo Mkoani Tabora
Akizungumza mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo Kanda ya Magharibi alisema katika kupata washindi vigezo vilizingatiwa kwa kutembelea mabanda yote yaliyoshiriki huku mazao na bidhaa zilizoletwa na wakulima na wafugaji zikizingatiwa, Hamasa katika Mabanda na matumizi ya Teknolojia katika Kilimo, mifugo na Uvuvi
Halmashauri, Kampuni, Taasisi za Serikali na serikali na vituo vya Utafiti vya mazao yatokanayo na kilimo, Mifugo na Uvuvi yalitunukiwa vyeti vya Ushiriki na Mgeni Rasmi huku waliotangazwa kutunukiwa vyeti vya ushindi
Aidha Mgeni Rasmi huyo akihutubia katika kufunga Maonesho hayo alisema Kanda ya Magharibi yaani Mkoa wa Kigoma na Mkoa wa Tabora kuna uwezekano wa kuwa wenyeji kwa maonesho ya kitaifa huku wakiwataka washiriki kujiandaa kikamilifu kuanzia sasa
Kwa picha zaidi tembelea Maktaba ya picha kwa kubofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa