Na Mwandishi Wetu
Wananchi na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kujiandaa na kushiriki sensa ya Watu na Makazi inayotarajia kufanyika August 23, 2022 ili kupata takwimu sahihi zitakayoisaidia Serikali kupanga Mipango ya Maendeleo
Yamesemwa hayo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi Jana July 14, 2022 wakati akifungua Mafunzo ya kupinga ukatili kwa Wanawake na Watoto yaliyofanyikia ukumbi wa Ndela kwa Viongozi wa dini, Waganga wa tiba Asilia, Wawakilishi wa Watu waishio na Virusi vya Ukimwi kutoka katika kata zote kumi na tisa ( 19) za Manispaa hiyo
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema umuhimu Sensa ya Watu na Makazi ni pamoja na Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa dira ya Maendeleo kwa Mwaka 2025, Mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendelo Kitaifa na Kimataifa, na Serikali kupata takwimu la Ongezeko la Watu itakayosaidia upangaji bajeti na Maendeleo kwa Wananchi
Alisema katika siku ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Watu Wote watahesabiwa kwa utaratibu uliopangwa ikiwemo Wasafiri watakaolala katika Vituo vya Kusafiria Kuamkia Siku ya Sensa na kwa kila Kaya zilizopo
Katika Mafunzo hayo aliwataka Washiriki wa Mafunzo hayo kuwa tayari kuhesabiwa na kuendelea kupinga vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika Jamii na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile Jeshi la Polisi na Ofisi za Ustawi wa jamii
Mafunzo mengine aliyoyahudhuria na kuyafungua ni Mafunzo ya kupinga ukatili wa Wanawake na Watoto kwa Vikundi vya Malezi chanya toka ngazi ya jamii ikihusisha Viongozi wa dini, Watu Wenye ulemavu, Makundi ya Vijana, Wawakilishi wa Mama na Baba bora, Watu maarufu kutoka Kata za Buzeba zeba, Katubuka na Kipampa yaliyofanyikia Shule ya Msingi Ujiji
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa