Na Mwandishi Wetu
Kituo cha afya kipya cha Buhanda kilichopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kilichojengwa kwa fedha za tozo (kodi) ya miamala ya simu Jana Novemba 08, 2022 kilifunguliwa kwa lengo la kuanza kutoa huduma za afya kwa Wananchi
Kituo hicho kilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe ambapo aliwataka Wananchi kutunza miundombinu ya kituo hicho ili kuwanufaisha Watu wengi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athuman Msabila alisema ujenzi wa Kituo hicho uliohusisha Jengo la Wagonjwa wa nje, Maabara na kichomea taka umegharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Millioni Mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu iliyotokana na kodi za miamala ya simu
Alisema Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya afya katika Manispaa hiyo na inatarajia kupokea kiasi cha fedha za Kitanzania Million mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya itakayojengwa Kata ya Kagera
Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa ujenzi wa jengo jingine la upasuaji na wodi ya wazazi unaendelea kwa fedha za Kitanzania Million mia mbili hamsini (Tsh 250, 000, 000/=) kutoka Serikali Kuu katika kituo hicho cha afya
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Hashimu Mvogogo alisema tayari wahudumu wa Afya watano (05) na Mganga wa Kituo hicho wamepangwa na huduma zitakazoanza kutolewa ni pamoja na huduma kwa wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na kupumzisha, huduma za dharura, huduma za kimaabara huku akisema kukamilika kwa miundombinu inayoendelea kujengwa kutaanza kutolewa kwa huduma ya upasuaji na huduma ya baba,Mama na mtoto
Naibu Meya wa Manispaa hiyo Bi. Mgeni Kakolwa aliwataka wahudumu wa Afya kufanya kazi kwa weredi kwa kuzingatia misingi ya kazi na upendo kwa Wananchi wanaowahudumia huku akiipongeza Serikali kwa uboreshaji wa miundombinu unaoendelea katika Manispaa hiyo
Diwani wa Kata ya Buhanda Mhe. Gilberth Kilahumba aliishukuru Serikali kwa kuendelea kujenga, kuboresha na kusogeza huduma mbalimbali kwa Wananchi kama vile Ujenzi wa Madarasa na miradi ya Afya katika Kata hiyo
Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Buhanda kunafanya Manispaa hiyo kuwa na jumla ya idadi ya vituo vya afya Vitatu (03) ikiwemo kituo cha afya cha Ujiji na kituo cha Afya Gungu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa