Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia sita sitini na mbili (Tsh 662,000,000/=) kwa ajili ya Ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Rusimbi.
Ujenzi huo unatarajia kufanyika katika eneo la Zahanati ya Rusimbi ambapo kituo hicho mara baada ya ujenzi wa Majengo kukamilika Zahanati hiyo itapanda hadhi na kuwa Kituo cha afya.
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho unatarajia kuwanufaisha Wakazi wa eneo na maeneo jirani kwa kujipatia ajira na kuboreshwa kwa huduma za matibabu.
Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuboresha huduma za afya kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ibara ya 81 inayoitaka Serikali Kuongeza Vituo vya afya ili Wananchi wawe na Afya bora na Kushiriki Shughuli za Maendeleo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa