Na Mwandishi wetu
Wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha mbolea za mazao kwa kuchakata taka kuanza kujengwa Desemba Mwaka huu Manispaa ya Kigoma/Ujiji, yameelezwa na Mhandisi mshauri Ndugu. Ahadi Katela kutoka Kampuni ya Gwavey Company Limited inayozalisha mbolea za urutubishaji mazao
Katika kikao hicho kilichofanyika leo April 30, 2021 katika hotel ya Sunset Vista iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kilichoandaliwa na shirika la utunzaji Mazingira ziwa Tanganyika(LATAWAMA) kikihusisha wakuu wa idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kikiwa na lengo la kutoa mrejesho wa utafiti wa uliofanyika wenye lengo ya kuhakikisha mji unakuwa safi
Mhandisi mshauri huyo amesema kampuni ya Gwavey Companya Limited inayozalisha mbolea inatarajia kufungua kiwanda cha kutengeneza mbolea za mazao ya wakulima ambapo watatumia uchakataji wa taka zitokanazo na mabaki ya vyakula na bidhaa zingine zinazozalishwa katika makazi na masoko ya Manispaa hiyo
amesema kwa mjibu wa utafiti uliofanyika masoko yaliyopo katika Manispaa hiyo yanazalisha kiasi kikubwa cha taka zinazofaa katika uzalishaji wa mbolea ya Mazao huku akitolea mfano wa soko la Nazareth linalokisiwa kuzalisha Tani 1000 kwa mwaka huku akisema ujenzi wa kiwanda hicho kitawanufaisha wakulima wa mkoa wote wa Kigoma
Naye Mtaalamu wa udhibiti wa taka ngumu na Mazingira Ndugu. Patrick Matandala amesema Manispaa ya Kigoma/Ujiji inawajibu wa kuhakikisha mji unakuwa safi kupitia watendaji kata na mitaa kusimamia maeneo yao kikamilifu huku vikosi kazi(CBOs) vikiimarishwa na kuhakikisha sheria ndogo za Mazingira zinafuatwa na watu wote
Mkurugenzi wa shirika la utunzaji Mazingira ziwa Tanganyika (LATAWAMA) Ndugu. Didier Cadelli amesema taasisi hiyo itaendelea kutoa vifaa vya kuwezesha na kuhakikisha mji unakuwa safi na kupunguza taka mjini kwa kuweka miundombinu imara ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vipuri vya magari na vifaa vya kuzolea taka (skip bucket) vinakuwa imara huku kampuni za mbolea nazo zikinufaika
Mganga mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Sebastiani Siwale akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo amelishukuru shirika la utunzaji Mazingira ziwa Tanganyika(LATAWAMA) kwa jitihada zao za kuendelea kufadhili vifaa vya kuendeleza usafi wa mji huku akisema Manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia wataalamu wako tayari katika kuhakikisha na kusimamia mji unakuwa safi na taka zinatumika kwa shughuli za uzalishaji wa mbolea na kuwanufaisha wakulima
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa