Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Saimoni Nyakoro Sirro amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi wa Soko la Mwanga kukamilisha ujenzi kwa wakati kutokana na kuongezewa mda wa Kazi.
Kiongozi huyo ametoa agizo hilo Leo Januari 07, 2026 alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa soko huku akisema Wananchi wanasubili kuanza kutumia Soko hilo.
Amemtaka Mkandarasi wa ujenzi kukamilisha ujenzi kwa wakati na kufikia mwezi May, 2026 awe amekabidhi mradi ili uanze kuwanufaisha Wananchi.
Akiwasilisha taarifa Mhandisi wa Ujenzi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Asabhi contractor Company Ltd in Jv with Pioneers Builders Limited Eng. Joseph Marando amesema uchelewaji wa mradi umetokana na changamoto ya Mvua kubwa mwanzoni mwa utekelezaji wa Mradi.
Amesema tayari wamepewa muda wa ziada wa Siku 115 na wanatarajia kukamilisha ujenzi April 24, Mwaka huu huku maendeleo ya ujenzi wa Mradi ukiwa Asilimia hamsini na moja (51.59%).
Serikali ya Awamu ya Sita inatekeleza Ujenzi wa Soko la Mwanga na Mwalo wa Katonga kwa thamani ya zaidi ya Billion kumi na Sita (Tsh 16,495,359,710.28/=) kwa lengo la kuboresha miundombinu, kukuza uchumi wa Wanannchi na huduma kwa jamii.
Kukamilika kwa Soko la Mwanga kutakuwa na maduka na vizimba, vyoo vya kawaida, vyoo vya walemavu, Vibanda vya chakula, Maegesho ya magari, Ofisi na Kituo cha Polisi kwa eneo la Jengo lenye Mita 23,872.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa