Na Mwandishi wetu
Wanawake wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kuripoti vitendo vya ukatili vinavyoweza fanywa na makundi mbalimbali ndani ya jamii ili kupata jamii yenye mafanikio kwa kulinda uchumi , kuwa na Mazingira salama na kulinda mila na desturi
Yamesemwa hayo leo March 8,2021 na Katibu Tawala Mstaafu ambaye alikuwa Mgeni Rasmi Bi. Magreth Heguye katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Mwananchi ambapo amesema vitendo vya ukatili kwa wanawake vinahafifisha maendeleo ya kiuchumi katika kufikia malengo yao
Aidha mgeni rasimu huyo amevitaka vyombo vinavyohusika na kupiga ukatili na kutoa haki kama vile Jeshi la Polisi, Mahakama na Ustawi wa jamii kuwasiliza wale wote wanaonyanyaswa na kufanyiwa ukatili ikiwa ni pamoja na kuwafungulia mashitaka ili haki ipate kutendeka
Awali akiwasilisha taarifa ya uwezeshaji katika kipindi cha miaka miwili Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Bernadetha Ntembeje amesema Halmashauri imeweza kutoa kiasi cha fedha Million mia moja tisini na nane mia tano elfu (198,500,000/=) kwa vikundi vya uzalishaji mali vya wanawake na jumla ya wanawake mia nane na arobaini walinufaika
Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Agnes Punjila akiwasilisha taarifa ya Mpango wa Kupinga Ukatili wa wanawake na watoto(MTAKUWWA) kwa Mwaka mmoja amesema kamati iliweza kusimamia mashauri ya Ukatili dhidi ya watoto ambapo ukatili wa kimwili ikiwa ni kupigwa na kuchomwa na vitu vyenye ncha kali matukio kwa watoto kumi (10) yalilipotiwa, Jumla ya matukio tisa (09) ya ukatili ya kingono yalilipotiwa, watoto waliotelekezwa wakiwa mia moja arobaini na moja (141), huku migogoro ya ndoa arobaini na saba (47) ikitatuliwa na mingine kufikishwa mahakamani
Aidha Afisa ustawi wa jamii huyo amesema katika shughuli hiyo changamoto wanayokumbana nayo ni pamoja na jamii kushindwa kutoa ushirikiano katika kutoa ushahidi mara kesi inapokuwa imepelekwa mahakamani hasa kesi za ubakaji na ulawiti
Afisa wa dawati la Jinsia na watoto wa jeshi la Polisi Merry Boniphace akiwatoa takwimu za makosa yaliyolipotiwa kwa kipindi cha mwezi January hadi February 2021 amesema vitendo vya kubaka matukio sita (06) yalilipotiwa na manne (04) yalipelekwa mahakamani, Mimba za utotoni kumi (10) zililipotiwa huku watu watatu (03) wakifikishwa mahakani na matukio ya shambulio yakiwa kumi na sita(16) na watu tisa (09) wakifikishwa mahakani
Ameendelea kusema takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka 2020 kulikuwa na makosa mengi ukilinganisha na mwaka 2021 na hakuna ongezeko la makosa ya ukatili kwa mwaka huu hali iliyosababisha na mwamko wa elimu kwa jamii juu ya kuzuia utendekaji wa makosa ya ukatili
Herena Jokali mwanamke na Mkazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji ameipongeza Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kuandaa maadhimisho hayo yanayowapatia elimu namna wanavyoweza kupinga ukatili na kujifunza mbinu za kujiinua kiuchumi katika Nyanja za biashara, kilimo, na usindikaji
Picha na video zaidi ingia Maktaba ya picha kwa kubofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa