Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imefanya maadhimisho ya Siku ya Maziwa kwa kuhamasisha Wananchi kuendelea kunywa Maziwa na kufanya maonesho ya bidhaa zitokanazo na maziwa.
Maadhimisho hayo yamefanyika yakihudhuriwa na Viongozi wa Serikali, Makundi ya Wafugaji, Wajasiriamali, Wanafunzi, na Wananchi.
Mgeni rasmi akihutubia Mkutano huo Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Mganwa Nzota amewataka Wananchi kutumia fursa ya maziwa kukuza Uchumi kwa kujiingizia kipato na Maafisa ugani kuendelea kuwajengea uwezo mbinu za Kisasa Wachakataji wa zao hilo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Wananchi kujitokeza kwa Wingi kufanya ufugaji wa ndani wa mifugo huku akisema maziwa ni Chakula, Biashara na ni dawa.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ina Jumla ya Ng'ombe wa maziwa 1255, Wanaokamuliwa wakiwa 972 na uzalishaji wa maziwa kwa siku ukiwa lita 5832.
Takwimu za Kitaifa zinaonesha unywaji wa maziwa bado upo chini zikionesha Mtu mmoja anakunywa lita 67.5 kwa Mwaka ambapo kiasi hitajika kwa Mwaka ni lita 200.
Kauli Mbiu ni "Maziwa Salama kwa afya Bora na Uchumi endelevu'.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa