Na Mwandishi Wetu
Maafisa elimu Kata na Walimu wakuu wa shule za msingi manispaa ya Kigoma Ujiji Jana January 30, 2025 wamehitimisha Mafunzo ya Siku tatu (03) yaliyoandaliwa na Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid.
Mafunzo hayo yaliyofanyikia Shule ya Msingi Kabingo yalilenga kujengeana uwezo na mahusiano mazuri katika kutatua changamoto za usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji kwa kuanzisha Jumuiya za kujifunza za Walimu wakuu na Maafisa elimu Kata (JZK)
Mpango wa uanzishaji jumuia unalenga kuendeleza mikakati ya kielimu na kukuza viwango vya ufaulu na kupunguza ufaulu wa madaraja ya chini kwa Wanafunzi wa Manispaa hiyo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa