Mkuu wa idara ya mipango miji Ndugu. Brown Nziku aanza na utekelezaji wa agizo la waziri mkuu kwa kusikiliza watu wenye malalamiko ya ardhi waliojitokeza na mabango siku ya jumamosi july 28, katika uwanja wa kawawa.
Mkutano huo uliofanyika jana katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji ikihusisha wataalamu sita(6) kutoka idara ya mipango miji , na afisa malalamiko wa halmashauri.
Katika mkutano huo ambao lengo ilikuwa ni kusikiliza malalamiko yaliyowasilishwa kwa waziri mkuu na kuandikiwa ripoti kwa kuwasilishwa mkoani hadi kwa ofsi ya waziri mkuu kwa kuelezwa namna ilivyoshugulikiwa.
viongozi kutoka Idara ya Mipango miji wakisikiliza malalamiko ya wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji yahusuyo migogoro ya ardhi ikiongozwa na mkuu wa idara Ndugu Brown Nziku(watatu kutoka kulia) wakiwa na afisa malalamiko wa halmashauri Ndugu. Mollel(kwa jina moja) wa kwanza kutoka kulia.
Mkutano huo uliochukua zaidi ya masaa matano kwa kusikiliza malalamiko ya mtu mmoja moja na makundi ambapo wataalamu ilikuwa wakisikiliza, kuyaratibu, kuyatolea ufafanuzi pamoja na kutoa ushauri kwa wateja (walalamikaji).
Malalamiko mengi yaliyojitokeza ni pamoja na watu wengi kutapeliwa viwanja na watu binafsi ambapo wataalamu hao kupitia kwa mthamini Ndugu. Steven Amblosi, mpima ardhi Bi. Halima Mmbaga wakiwa na afisa malalamiko Mollel waliweza kutoa ushauri kwa kuwashauri kupeleka masuala hayo kupitia vyombo vya kisheria ikiwa ni pamoja na mahakama pamoja na polisi.
wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji wakiwasikiliza viongozi wa idara ya mipango miji kuhusu malalamiko ya ardhi wa kwanza mkono wa kushoto ni mzee Abeid Mzee Karubi
Katika kuendelea kusikiliza malalamiko ya wakazi hao wa manispaa ya Kigoma/Ujiji suala lingine lililojitokeza ni malalamiko kuletwa ambayo tayari yapo katika vyombo vya kisheria jambo ambalo wataalamu hao wamewashauri wateja wao kusubili uamuzi wa vyombo hivyo vya kisheria huku wakieleza kutokuwa na mamlaka ya kuingilia vyombo hivyo.
Malalamiko mengine yaliyojitokeza ni pamoja na baadhi ya Taasisi kujengwa katika viwanja vya watu bila kulipwa fidia yeyote jambo ambalo wataalamu hao wa masuala ya ardhi wameteua timu kwa ajili ya ufatiliaji malalalamiko hayo baada ya mkutano huo na mengine kuyaratibu na kuyapeleka mkoani na hatimaye kutumwa ofsi ya Waziri mkuu.
Mkutano huo uliochukua takribani masaa matano katika ukumbi wa halmashauri ukiwa umehudhuliwa zaidi ya watu hamsini ambapo mkuu wa idara ya mipangomiji Ndugu Brown Nziku amewashukuru watu wote walioitia mkutano huo pamoja na wataalamu kwa kuwasikiliza wateja, na kuahidi malalamiko hayo watayafanyia kazi kwa kutumwa mkoani na mkoani kuyawasilisha ofsi ya waziri mkuu.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa