Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Leo May 07,2025 ameongoza Kamati ya Usalama ya Wilaya kukagua miradi ya maendeleo Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikiwa ni Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025.
Kamati hiyo imekagua Ujenzi wa Ukumbi wa Kisasa unaoendelea eneo la Mwanga Centre kupitia Mapato ya ndani kwa gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billion tatu (Tsh Billion 3/=), Ujenzi wa Zahanati mpya Kata ya Rubuga kupitia mapato ya ndani kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million Mia moja na thelathini (Tsh 130,000,000/=), Ujenzi wa Ofisi za Kata ya Kasimbu na Kigoma kupitia Mapato ya ndani.
Kamati hiyo imekagua Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kata ya Kipampa kwa gharama ya fedha za Kitanzania Million Mia sita na tatu (Tsh 603,000,000/=), Ujenzi wa nyumba ya Walimu Shule ya Sekondari Mjimwema, Ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule ya Sekondari Buronge na Kikundi cha Vijana cha uchomeleaji Kata ya Gungu.
Mkuu wa Wilaya amewataka Wataalamu kuendelea kusimamia kwa ukaribu miradi inayoendelea kujengwa ili kuleta tija kwa Wananchi, Aidha Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kigoma/Ujiji unatarajiwa kukimbizwa Septemba 21 Mwaka huu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa