Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Leo Februari 20, 2025 amefanya kikao cha maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka huu.
Kikao hicho kimefanyikia Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Kikihudhuriwa na Kamati ya Usalama, Wakuu wa taasisi, Wakuu wa Idara, Vitengo na Kamati za Maandalizi.
Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na aliyekuwa Mkimbiza Mwenge Kitaifa Mwaka 2024 Ndugu. Makwaya Makwaya ambapo ametoa nasaha ya maandalizi kwa Mwaka huu.
Kikao hicho kimejadili tathimini ya Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2024 ambapo Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilishika nafasi ya pili(02) Kimkoa, Nafasi ya nane (08)kikanda na Kitaifa nafasi ya sitini na tatu (63) Kati ya Halmashauri 195 Nchini, huku kikao hicho kikijadili maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Septemba 21, Mwaka huu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa