Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imezindua sherehe za miaka sitini (60) ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi katika soko la Buzebazeba na upandaji Michikichi kando ya barabara ya Mwasenga
Uzinduzi huo umefanyika ukiongozwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe ambapo ameshiriki shughuli hizo
Mkuu huyo wa Wilaya akiwa katika soko la Buzebazeba amewataka wafanyabiashara wa soko hilo kuzingatia suala la Usafi ili kudumisha afya zao na wanunuzi wa bidhaa kwa kuzuia milipuko ya Magonjwa inayoweza kutokea
Ameendelea kusema Upo mkakati wa kuanzisha mashindano ya Usafi wa Masoko ili kuhakikisha usafi unadumishwa na masoko yanakuwa rafiki katika shughuli za Kiuchumi
Aidha amewataka kuhakikisha wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wanapanda miti ya Zao la Michikichi ili kutunza Mazingira na kupata faida ya mazao ya kiuchumi kama ambavyo Rais wa Awamu ya Kwanza na Mpigania Uhuru Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere alipigania suala la Utunzaji wa Mazingira
Mkuu huyo wa Wilaya amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Desemba 9, ambapo kutakuwa na maonesho kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kuonesha bidhaa zao katika Uwanja wa Mwanga Community Centre na Michezo mbalimbali ikifanyika kwa makundi mbalimbali wakiwemo Wazee, Vijana, na Watoto
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema "Kuharibu Mazingira ni kuiba mali ya Vizazi ambavyo havijazaliwa, Ni kudhulumu haki ya Watoto na Wajukuu wa vizazi vijavyo, Mazingira mazuri tuliyonayo ni urithi kutoka vizazi vilivyotangulia, Hivyo ni Wajibu wa kuyalinda na kuyatunza Mazingira yetu "
Tanzania husherehekea Maadhimisho ya Uhuru Desemba 9, kila Mwaka ambapo Mwaka 1961 Tanzania wakati huo Tanganyika ilipata Uhuru kutoka kwa wakoloni Waingereza
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa