Na Mwandishi wetu
Machinga wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi soko la Mwanga leo October 29, 2021 wamepangiwa na kugawiwa maeneo ya kufanyia biashara zao eneo la seremala lililotengwa kwa ajili ya wajasiriamali hao huku wakipongeza utaratibu uliotumika katika zoezi hilo
Akizungumza wakati wa kuwapangiwa machinga hao, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe amesema zoezi hilo limefanyika kwa njia Shirikishi ambapo viongozi wa machinga wamekuwa wakishiriki katika kila hatua ya kupangiwa maeneo ya kibiashara yaliyoboreshwa ikiwa ni pamoja na kupata majina ya wafanyabiashara wadogo (Machinga)
Mkuu wa Wilaya amesema kabla ya zoezi hilo Ofisi ya biashara Manispaa ya Kigoma/Ujiji ilipokea majina ya wafanyabiashara wadogo (Machinga) Mia nne themanini na Sita (486) waliojiandikisha kwa viongozi wao huku maeneo yaliyopimwa katika eneo hilo yakiwa Mia nne tisini na Sita (496)
Mkuu wa Wilaya ameendelea kusema hakutakuwa na viashiria vya upendeleo katika kupata maeneo ya biashara ambapo utaratibu wa kusoma majina kwa kuchukua karatasi zenye namba ya eneo la kufanyia biashara ndilo litakalotumika kwa kila Machinga
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athumani Msabila amewataka wafanyabiashara hao wadogo (Machinga) kuhakikisha wanatunza Mazingira katika eneo hilo jipya kwa kutokutupa taka ovyo na kuhakikisha kanuni za afya zinazingatiwa huku akisema miundombinu katika eneo hilo itaendelea kuboreshwa
Baadhi ya viongozi wa Machinga wa soko la Mwanga akiwemo Ndugu. Ali Jafari amesema zoezi hili limekuwa Shirikishi tangu hatua ya kwanza kwa kufanya vikao na Mkuu wa Wilaya na kusema wao kama viongozi ndio wameshiriki kuandika majina ya machinga wote pasipo kuwa na upendeleo
Nao baadhi ya Machinga akiwemo Bi. Agnes na Madua Ahamadi wamepongeza zoezi lilofanyika katika kupata maeneo ya biashara zao huku wakisema njia hiyo ya kuandika namba za viwanja na machinga kuchukua karatasi hizo zinaondoa migigoro ya wengine kuona wamependelewa
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa