Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Samson Anga leo January 14, amefungua mafunzo ya Uongozi kwa Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji namna ya kusimamia na uendeshaji wa serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Hoteli ya Gronecy iliyopo Halmashauri ya Mji Kasulu
Akifungua Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Wataalamu na wakufunzi kutoka Chuo cha Hombolo Mkuu wa Wilaya huyo amewataka Waheshimiwa Madiwani Mafunzo watakayoyapata kuwa na Nidhamu ya kusimamia mabaraza, na Nidhamu ya kusimamia fedha za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa ili kufikisha Maendeleo kwa Wananchi
Amehitimisha kwa kuwataka Waheshimiwa Madiwani kutoa Ushirikiano katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kuhakikisha na kufikia Malengo na Utatuzi wa Changamoto za Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Naye Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Lupoĺi akizungumza katika Ufunguzi huo amesema Mafunzo hayo yataboresha utendaji kazi kwa Madiwani katika kutatua changamoto na kuleta Maendeleo kwa Wananchi katika Kipindi watakachokuwa Madarakani
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Hiyo Ndugu. Frednand Filimbi akizungumza amesema Mafunzo hayo yataendeshwa kwa mda wa siku tatu (03) na yanatarajiwa kuleta matokeo Chanya katika kuleta Maendeleo kwa Wananchi na wakazi wa Manispaa hiyo kutokana na Mada zitakazowasilishwa huku akisema mafunzo hayo kufanyika Nje ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ni kuhakikisha Walengwa wa Mafunzo hayo kutotoa na kufhibiti Udhuru kwa walengwa wa Mafunzo hayo
Katika Mafunzo hayo yaliyohudhuliwa na Wakuu wa Idara na Vitengo, Madiwani na Viongozi wa vyama vya siasa mada kumi (10) zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa ni pamoja na 1. Uongozi na Utawala Bora, 2.Historia , Uhalali na sheria za Uendeshaji wa serikali za Mitaa 3. Muundo, Majukumu, na Madaraka ya Serikali za Mitaa 4.Muundo na Majukumu ya Uendeshaji wa Vikao na Mikutano ya serikali za Mitaa, 5. Usimamizi na Udhibiti wa Fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 6. Usimamizi wa Mikataba ya Manunuzi 7. Usimamizi wa Ardhi katika Serikali za Mitaa 8.Usimamizi wa Watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, 9. Usimamizi wa Miradi ya Kimkakati na 10. Wajibu, Majukumu, Haki na Stahiki za Diwani
Picha zaidi ingia Maktaba ya Picha www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa