Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Uchumi, elimu, na Afya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo May 03, 2023 imefanya ziara ya kutembelea Mtaa wa Mgumile kata ya Kagera kwa lengo la kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa Zahanati
Źiara hiyo imefanyika ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Gregory Keberezo ambapo viongozi hao wamefika na kukagua eneo kwa lengo kusogeza huduma za matibabu karibu na Wananchi
Wananchi wa Mtaa wa Mgumile wamekuwa wakitembelea takribani Km 8 kufuata huduma za Matibabu katika kituo cha afya cha Ujiji Kilichopo kata ya Kasimbu, Hivyo ujenzi wa Zahanati hiyo itakuwa na manufaa kwa Wananchi wa eneo hilo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa