Na Mwandishi Wetu
Madiwani wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo April 12, 2023 wamepongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya huduma za jamii kwa kutumia mapato ya ndani
Pongezi hizo zimetolewa Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupokea taarifa za Kata kwa robo ya pili Oktoba-Desemba, 2022/2023 uliofanyikia ukumbi wa Manispaa hiyo
Wakizungumza katika baraza hilo Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini Mhe. Mussa Mauldi na Diwani wa Kata ya Machinjioni Mhe. Shabani Hussein wamepongeza uongozi wa Manispaa hiyo kwa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kupitia vyanzo vya fedha kwa mapato ya ndani
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Athuman Msabila amewataka Madiwani hao kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea katika Kata mbalimbali kwa fedha zinazotolewa kupitia fedha za mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali Kuu
Baadhi ya miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa mwaka 2022/2023 kupitia mapato ya ndani ni pamoja na Ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Kitongoni, Ujenzi wa Zahanati ya Mwanga kusini, Ujenzi wa Zahanati ya Machinjioni, Ujenzi wa Ofisi za Kata Katubuka, ofisi ya Kata ya Majengo , na Ofisi ya Kata ya Buhanda
Aidha miradi mingine ni pamoja na Ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika Shule za Msingi za Benjamini Mkapa, Shule ya Msingi Kitongoni, Shule ya Msingi Majengo na Shule ya Msingi Gungu pamoja na utoaji Mikopo ya asilimia kumi (10%) kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa