Na Mwandishi Wetu
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametoa pongezi kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa namna inavyoendelea kutekeleza miradi ya Maendeleo kupitia mapato ya ndani
Pongezi hizo zimetolewa Katika Mkutano wa baraza la Madiwani la kupokea taarifa za Kata lilofanyika Leo Septemba 06, 2023 likiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Mgeni Kakolwa
Wakiwasilisha taarifa za Kata wanazoziongoza katika Mkutano wa baraza Diwani wa Kata ya Buhanda Mhe. Kilahumba Ruturi na Diwani wa Kata ya Machinjioni Mhe. Shabani Hussein wameipongeza ofisi ya Mkurugenzi kwa namna ilivyotekeleza na inavyoendelea kutekeleza Ujenzi wa miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani ikiwemo ofisi za Kata pamoja na Zahanati
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imetekeleza ujenzi wa ofisi za Kata za kisasa kwa mapato ya ndani ikiwemo Kata ya Buhanda, Majengo, Mwanga Kusini, Kata ya Katubuka na Ujenzi wa Zahanati ya Machinjioni
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa