Na mwandishi wetu.
Baraza la madiwani la manispaa ya Kigoma/Ujiji juzi ijumaa February 8, liliweza kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 kiasi cha Tsh 35,175,030,076.00.
Katika baraza hilo lililoanza majira ya saa nne asubuhi chini ya mwenyekiti na Meya wa manispaa hiyo Hussein Rihava na katibu Kaimu Mkurugenzi manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Bennert Ninalwo, ambapo mwenyekiti alianza kwa kuwakaribisha wajumbe wa kikao hicho na kuwa na ushirikiano kwa kuhakikisha wanatoa mapendekezo yatakayo saidia katika utekelezaji wa bajeti.
Akiwasilisha bajeti hiyo hiyo kwa baraza hilo la madiwani Mchumi wa Mipango,Uchumi na Takwimu Ndugu. Filimbi(kwa jina moja) alitoa mchanganuo wa bajeti akisema kiasi cha shilingi 2,042,533,234.00 ikiwa ni mapato ya ndani (OS), shilingi 923,934,000.00 ni ruzuku toka Serikali kuu , shilingi 24,941,741,000.00 ni ruzuku ya Mishahara, na shilingi 7,266,781,842.00 ni fedha za miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani na wafadhili, huku akimtaka Mwenyekiti wajumbe wake kuridhia kiasi hicho cha bajeti.
Nao madiwani walipata wasaa wa kujadili bajeti hiyo, moja ya mjumbe na Diwani wa Kata ya Kibirizi mhe. Ruhomvya akijadili bajeti hiyo aliweza kutoa mapendekezo kwa kueleza ili bajeti iweze kutekelezwa ni lazima makusanya ya mapato ya ndani yakusanywe ipasavyo na watumishi wa halmashauri na hasa katika minara ya makampuni ambayo ipo katika maeneo ya halmashauri huku akitaka bajeti hiyo inatoa kipaumbele kwa kutenga fedha kwa sekondari ya ya Upili Kasingirima na kuwa na madarsa ya kidato cha tano na sita.
Naye mwenyekiti wa kamati ya Elimu uchumi na Afya na diwani wa kata ya Kigoma mjini Mhe. Hussein Kariango, akichangia bajeti hiyo alisema Manispaa kupitia wataalamu wake waweke mipango dhabiti ya kuhakikisha chanzo cha mapato cha vibali vya ujenzi kinasimamia kwa uzuri katika kuongeza fedha za ndani kwa lengo la kutekeleza bajeti hiyo huku akiwataka wataalamu kuendeleza vyanzo vingine vya mapato kwa soko la Mwasenga, soko la Ujiji na Standi ya Ujiji kwa kuweka mazingira na miundombinu inayofaa huku akikumbusha fedha zinazodaiwa na madiwani wa halmashauri hiyo.
Baada ya kujadili bajeti hiyo madiwani waliweza kupitisha bajeti hiyo na mwenyekiti wa kikao hicho akitoa nafasi kwa Kaimu Mkurugenzi wa manispaa alieleza kuwa wataalamu wamepania katika kukusanya fedha na kuhakikisha madeni yote yanalipwa “milioni 30 zimetengwa kwa ajili ya madiwani tutahakikisha tunalipa madeni yote labda shetani atupitie” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.
Naye Naibu meya wa manispaa hiyo Athumani Athumani aliwataka wataalamu kuhakikisha wanasimamia mapato na kuhakikisha wanatoa taarifa ya madiwani ambao sio waaminifu katika kuingilia na kukwamisha ukusanyaji wa mapato huku akiwataka pia wataalamu kutowaona madiwani kama mazezeta.
Naye mwenyekiti wa kikao hicho na meya wa manispaa aliwashukuru madiwani kwa michango yao katika kujadili bajeti na kueleza bajeti hiyo ni mwisho katika uongozi wao kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu 2020 akiwataka madiwani kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata zao na halmashauri kwa ujumla.
PICHA ZAIDI INGIA KATIKA MAKTABA YA PICHA
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa