Na Mwandishi Wetu
Kamati za maafa ambazo pia ni timu za dharura Mkoani Kigoma zimeendelea kupata Mafunzo na kujengewa uwezo juu ya masuala ya kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko ikiwa ni Siku ya tatu (03) tangu mafunzo hayo kuanza.
Mafunzo hayo yameendelea Halmashauri ya Mji wa Kasulu yakitolewa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na Wataalamu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kakonko.
Mafunzo haya yanafanyika chini ya mradi wa Afya moja unaofadhiliwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ukitolewa kwa Wataalamu wa Sekta Afya, Mifugo, Maliasili, Mazingira, Waratibu wa Maafa, Wataalamu wa Maabara na Wataalamu wa Mawasiliano.
Mada zilizowasilishwa Leo April 18, 2024 ni pamoja na ukusanyaji, usafirishaji na upimaji wa sampuli katika Maabara, Usalama wa Mhudumu wa Afya, Jamii na Ulinzi wa Sampuli.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa