Na Mwandishi Wetu
Mafunzo ya Siku tatu (03) ya Maafisa elimu Kata, Walimu Wakuu , na Wenyeviti wa Shule za Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji yaliyokuwa yakiendeshwa na Wataalamu wa Elimu ngazi ya Halmashauri yamehitimishwa Leo March 02, 2023
Mafunzo hayo yalikuwa yamelenga kuwashirikisha Jamii , Wazazi na Walezi (UWAWA) katika kuinua viwango vya taaluma Shuleni
katika mafunzo hayo Wawezeshaji hao wamesema Jamii, Wazazi na Walezi katika masula ya kielimu wanawajibu wa kufanya na kuhudhuria vikao Shuleni, usimamizi na usomaji wa Wanafunzi nyumbani, kuibua na kuendeleza vipaji vya Wanafunzi pamoja na kuhamasisha uandikishaji, mahudhurio na Mvuko wa Wanafunzi
Wajibu mwingine ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa Jumla na maendeleo ya Shule , kusimamia Ustawi , usalama na kusimamia ujumuishi wa Wanafunzi kwa kushughulikia Vitendo vya ukatili, na ukiukwaji wa haki za Watoto na kutatua changamoto Za Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu
Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwa ni pamoja na Usimamizi wa rasilimali za Shule, Mapitio ya Matokeo ya Mitihani ya Darasa la nne na la Saba Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Ushiriki wa Jamii katika ukuzaji wa elimu
Kikao hicho kimeandaliwa na Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza Kupitia Mfuko wa UK aid kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kuwawezesha Viongozi wa Elimu ngazi za Kata na Shule kufanya Umoja wa Wazazi na walezi (UWAWA) katika shughuli za ufundishaji na ujifunzaji
#SHULEBORA #shulebora @plan_tanzania
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa