Na Mwandishi Wetu
Walimu na wasimamizi wa elimu ngazi ya kata wametakiwa kuibua hadithi za mfanikio za kujifunza kwa mfano kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa Wanafunzi katika mafunzo ya Siku mbili (02) yaliyoanza Leo Desemba 04, 2022 katika Shule ya Msingi Muungano
Ameyasema hayo Mkuza mitaala kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania Ndugu. Hwago Hassan Hwago alipokuwa akitoa mafunzo kwa Walimu waliopo kazini (MEWAKA) yakihusisha Wasimamizi wa elimu ngazi ya kata na Walimu wa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Mwanga Kusini na Kata ya Mwanga Kaskazini
Amesema hadithi za mafanikio ya kujifunza kwa mfano zinasaidia kutatua changamoto za ufundishaji na ujifunzaji, kutia moyo katika utendaji kazi, kuamsha ari ya kutenda kazi, na kukuza ushirikiano miongoni mwa wadau wa elimu
Amesema hadithi za mafanikio za kujifunza kwa mfano zinapatikana miongoni mwa Walimu, Jamii, Taasisi za Elimu, Viongozi wa dini, Wanasiasa na Wadau wote wa elimu
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mradi wa Shule unaofadhiliwa na mfuko wa Uk aids chini ya Usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Miradi wa Shule bora unatekelezwa katika Mikoa tisa (9) Nchini Tanzania ukihusisha Halmashauri sitini na saba (67) na Shule elfu tano mia saba hamsini na saba ( 5, 757) na Unatarajia kuwanufaisha Wanafunzi zaidi ya Milioni tatu na laki nane ( 3, 800,000) na Walimu zaidi ya elfu hamsini na nne ( 54, 000)
Mikoa inayotekeleza mradi wa Shule bora ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Katavi, Dodoma, Mara, Pwani, Rukwa, Simiyu, Singida na Mkoa wa Tanga
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa