Na Mwandishi Wetu
Walimu na wasimamizi wa elimu ngazi ya kata jana Desemba 11, 2022 walihitimisha mafunzo ya siku mbili (2) yaliyokuwa na lengo la kuwawezesha walimu kuibua hadithi za mafanikio za kujifunza za mfano zinazopatikana miongoni mwao ili kutatatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji ili kuinua ubora wa elimu nchini
Mafunzo hayo yaliendeshwa katika taasisi ya Ahlulbayt Islamic Centre yakihusisha Watendaji Kata, Waratibu Elimu Kata, Walimu Wakuu, na Walimu Wataaluma wa Shule za Msingi zilizopo Kata za Majengo, Kipampa, Businde na Rusimbi
Katika mafunzo hayo Watendaji kata walijadiliana na Walimu namna bora ya Ukuzaji elimu na ufaulu kwa kushirikisha Wazazi na Wadau wengine wa elimu katika maeneo yao
Aidha katika mafunzo hayo walijifunza namna kuibua hadithi za mafanikio za kujifunza kwa mfano kwa lengo la kuboresha ufundishaji na ujifunzaji
Mkufunzi na Mkuza mitaala kutoka taasisi ya elimu Tanzania Ndugu. Hwago Hassan Hwago alisema kutumia hadithi za mafanikio katika kufundisha na kujifunza zitamfanya mwanafunzi kuwa mbunifu ambapo atakuwa na uwezo wa kuibua tatizo, Ufumbuzi wa tatizo na kupata matokeo yaliyo bora
Mafunzo haya ya mradi wa Shule bora yanaendelea katika Halmashauri za Mikoa ya Kigoma, Singida, Katavi na Pwani kwa lengo la kukuza viwango vya elimu katika Mikoa hiyo yakiandaliwa na Mradi wa Shule unaofadhiliwa na mfuko wa Uk aids chini ya Usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa