Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema Halmashauri tayari imeanza kulipa fidia ya mimea kwa maeneo ambayo Wananchi walipisha kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu ya huduma kwa jamii.
Aliyasema hayo Jana Februari 12, 2025 alipofanya mkutano na Wananchi wa Kata ya Kagera uliolenga kujadili maendeleo ya Kata hiyo.
Aliitaka Ofisi ya Uchumi kushughulikia fidia ya mazao inalipwa ndani ya wiki moja kwa Wananchi waliotoa maeneo yao ya kujenga Shule ya Sekondari Wakulima kutokana na uthamini ambao umeshafanyika.
Aliendelea kusema Serikali inatarajia kuongeza miundombinu ya majengo zaidi ya ishirini na mbili katika Hospitali ya Manispaa iliyopo Kata ya Kagera huku akisema Mwezi Aprili, Mwaka huu Manispaa italipa fidia ya ardhi kwa Wananchi ili kupisha ujenzi katika Hospitali hiyo.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa