Wakazi na wanawake wa manispaa ya kigoma ujiji siku ya jumanne august 7,wameahidi kunyonyesha watoto kila inapohitajika na kuachana na tabia za kuogopa kutepeta kwa maziwa ili waweze kuondoa suala la udumavu na kukuza afya za watoto kimwili na kiakili.
Wameyasema hayo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani ambapo huadhimishwa tarehe 1-7 august kila mwaka, na kwa manispaa ya Kigoma/Ujiji yamefanyika katika kata ya businde ikihudhuliwa na wanawake pamoja na wanaume katika ukumbi uliopo jirani na zahanati ya kata hiyo maarufu kama ukumbi wa Rich.
Katika ukumbi huo semina na mafunzo ya unyonyeshaji yaliyofanyika yakiongozwa na Afisa lishe manispaa ya Kigoma/Ujiji bi. Naomi Rumenyera wanawake wamekili kuendelea kunyonyesha kwa wakati na kila mara mtoto anapo hitaji kunyonya, akichangia mada mama aliyejitambulisha kama mama Suzi makala, amesema limekuwepo tatizo kubwa la unyonyeshaji la akina mama kutokana na harakati na shuguli za maisha huku wengine wakiogopa kuwa endapo wangenyonyesha matiti yangeanguka, kulala na kutepeta jambo linalofanya baadhi ya wanaume kutowapenda tena na wengine kukosa wanaume wa kujenga nao mahusiano mengine.
Katika semina hiyo iliyoongozwa na Afisa lishe bi.Naomi Rumenyera akiwa na kaimu Afisa chanjo manispaa, afisa maendeleo ya jamii na wadau wengine waliojitokeza akiwemo afisa kutoka taasisi na asasi ya Ndela iliyopo katika manispaa hiyo, afisa lishe huyo amesisitiza kwa kueleza umuhimu wa wa maadhimisho hayo na malengo ya siku hiyo ikiwa ni pamoja na uhusiano uliopo baina ya lishe bora,uhakika wa chakula, kupunguza umasikini na unyonyeshaji, unyonyeshaji kama msingi wa maisha lakini pia afisa lishe huyo aliendelea kuonesha umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee chini ya kabla ya miezi sita.
Aliendelea kusema unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni jukumu la watu wote katika jamii kuhusika ikiwa ni pamoja na wakuu wa masuala ya ulishaji wa watoto wachanga na wadogo, watunga sera, vyombo vya habari, wanawake na watoto, familia na jamii kwa ujumla , kwa kusema watu wote hao watakapohusika suala la udumavu kwa watoto litakungua kwa kiasi kikubwa na kuzuia aina zote za utapiamlo kwa watoto pamoja na wazazi ,lakini pia kuondoa na kupunguza hali ya umasikini kwa kusema kama watoto watanyonya kwa utaratibu watakuwa na akili nzuri ambazo zitawafanya kufikiri na kuwa wabunifu jambo litakalo fanya kuondoka na kupungua kwa umasikini kutokana na ubunifu na akili zinazofikiri.
Afisa lishe huyo akiendelea kutoa semina hizo aliongea na wanaume waliohudhulia katika ukumbi huo kwa kuwataka kuhakikisha kuna mazingira rafiki katika unyonyeshaji kama kutoleta migogoro majumbani kwa wanyonyeshaji jambo linalosababisha mawazo na kusababisha maziwa kutoweka na kutotoka kutokana na migogoro jambo ambalo ni hatari kwa afya ya mtoto.
mwanamke alipokuwa akinyonyesha katika ukumbi wa kata ya Businde maarufu kwa jina la ukumbi wa Rich katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya unyonyeshaji duniani august 1-7.
Lakini pia aliendelea kuwataka wanaume hao kuhakikisha uwepo wa chakula cha kutosha kwa mama mnyonyeshaji ili maziwa yaweze kuzalishwa kwa wingi na kufanya kuimarika kwa afya ya mama na mtoto na kufanya kuwa na kizazi imara kwa mstakabali wa maendeleo ya manispaa na taifa kwa ujumla.
Naye baba aliyejitambulisha kwa jina moja Ndugu. Shabani akiwa na uzoefu wa miaka arobaini katika malezi ya watoto amesema zipo changamoto kadhaa zinazojitokeza kwa akina baba , baadhi ikiwa ni pamoja na migogoro ya kifamilia jambo ambalo linaathiri afya kwa akina mama na watoto kwa ujumla katika kipindi cha unyonyeshaji ambapo amekiri na kuwataka wanaume waliohudhulia semina hizo kufanya mabadiliko na kuwa mawakiri kwa wanaume wengine lakini pia kwa kuwataka wanaume kujibidisha katika uzalishaji ili kuweza kuleta matoke chanya ya kifamilia kwa kuhakikisha uwepo wa chakula ili kuimarisha afya ya mama mnyonyeshaji na afya ya mtoto.
Akiendelea kutoa semina hizo Afisa lishe bi. Naomi Rumenyera ametoa takwimu kutokana na Utafiti wa Hali ya Afya na Demografia wa mwaka 2015/2016 amesema tafiti hizo zilionesha kati ya wanawake10 wanaonyonyesha , wanawake 5 tu ndio hunyonyesha watoto wao katika saa moja ya mwanzo na wanawake 6 kati ya 10 huendelea kunyonyesha maziwa ya mama ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo. Na kuwataKa wafanyie kazi kile kinachopaswa katika unyonyeshaji.
Naye afisa maendeleo manispaa ya Kigoma Ndugu. Jabiri Majidi katika semina hizo ameeleza faida za unyonyeshaji na hasara za kushindwa kunyonyeza maziwa pekeeya mama mtoto miezi sita ya mwanzo na athari zinazotokana na mtoto kupewa chakula kabla ya miezi sita ya mwanzo
Moja ya athari alizozieleza afisa maendeleo huyo mama anaposhindwa kunyonyesha huweza kuleta athari hasi kwa mama hata kwa mtoto pia kama vile kupata saratani ya matiti kwa mama, kutungwa kwa mimba mapema katika umri mdogo wa mtoto aliyezaliwakutokana na kurudi siku zake mapema baada ya kujifungua na athari alizozieleza ambazo mtoto anaweza kupata pindi atakaposhindwa kunyonya maziwa ya mama katika miezi sita ya awali ikiwa ni pamoja na magonjwa kwenye njia ya hewa, kuharisha, kiribatumbo pamoja na kisukari.
Katika uelimishaji na semina hizo zilizofanyika kwa lengo la kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji afisa lishe aliwataka waliohudhulia wote kuhakikisha kuyafanyia kazi na hata ujumbe huo kuwafikishia wanaume na wazazi wengine hawakupata elimu kwa kuhakikisha kila mmoja anauwa balozi kwa mwenzake katika kutoa uelimishaji huo. Baada ya kutoka kata ya Businde maafisa hao na wataalamu hao wameenda kutoa uelimishaji huo katika kata ya Rusimbi kwa kukutana na vikundi mbalimbali vya wanawake wakiwemo wajasiliamali ambapo semina hizo zilifanyika katika shule ya msingi Kipampa.Na kitaifa maadhimisho hayo yalifungulia august 1, 2018 na mgeni rasmi akiwa ni waziri wa afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto mhe. Ummy Mwalimu.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa