Na Mwandishi wetu
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi leo june 25 amesema Manispaa hiyo itagawa vifaa vya kujinga and Ugonjwa wa Corona Kwa shule zote za msingi na sekondari mara tu baada ya wanafunzi kufungua shule
Ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo kutoka kwa taasisi ya Direct Aid Society vyenye thamani ya fedha za Kitanzania Shilingi Million saba (Tsh 7,000,000/=) inayojishughulisha na kutoa misaada kwa jamii za wahitaji
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kama Manispaa tayari wameweka mpango na vifaa ambavyo watasambaza Mashuleni mara tu wanafunzi watakapokuwa wameanza masomo yao huku akisema msaada huo walioupokea wa Barakoa, Sabuni ,vitakasa mikono, gloves na vipima joto vitaongeza nguvu kuendelea kusambaza katika taasisi za shule na vituo vya kutolea afya
Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo tawi la Kigoma Ndugu Mohamed Arab amesema katika kipindi cha ugonjwa wa Corona wamekuwa na utaratibu wa kuifikia jamii kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo ambapo mwezi May, Mwaka huu kampuni hiyo iligawa msaada wa vyakula katika vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma uliogharimu fedha za Kitanzania Shilingi Million ishirini (Tsh 20,000,000/=)
Mkurugenzi huyo amehitimisha kwa ķuishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa misaada wanayokuwa wanaitoa ya kuihudumia jamii huku akisema wataendelea na ushirikiano kwa kufika katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na maeneo mengine ya Mkoa wa Kigoma
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr.Tibezuka Zinga amesema idara ya afya tayari iko tayari kwa ajili ya kutoa msaada wa Kisaikolojia kwa wanafunzi watakaoanza masomo yao siku ya Jumatatu june 29 kwa shule zote za Msingi na Sekondari zilizopo katika Manispaa hiyo
Ameendelea kuwasisitiza na kuwataka wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuchukua tahadhari ya kujikinga na Ugonjwa huo kutokana na kupungua Nchini kwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono kila mara , na kuvaa barakoa
March 17, Serikali ilitangaza kufungwa kwa shule na vyuo kutokana na idadi maambukizi ya Virusi vya korona, kutokana na kampeni iliyoongozwa nchini ya Kuliombea Taifa na kampeni ya kujifukiza maarufu kwa jina la "Kupinga Nyungu" virusi vya corona vimeendelea kupungua Nchini ambapo June 16, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr John Pombe Magufuli akihutubia hotuba ya kulifunga Bunge la 11 alitangaza June 29 shule za Msingi na Sekondari kuanza Masomo yao
Rais Magufuli Alisema ''Namshukuru Mungu kwa kuliepusha taifa hili na virusi vya corona na nina washukuru viongozi wa dini kwa kuitika wito wa serikali kufanya maombi maalum ya kutuepusha na janga la corona.''
''Kutokana na kushuka kwa hali ya maambukizi ya ugonjwa wa corona napenda kutumia nafasi hii kutangaza kuwa shule zote zilizokuwa zimebaki zifungulliwe, lakini pia shughuli zote zilizokuwa zimezuiwa nazo ziendelee'', huku akiendelea kuwasihi Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa