Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji Jana March 06, 2023 ilifanya kongamàno na mdahalo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
Kongamano hilo lilifanyikia Ukumbi wa Ndela ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa March 01- 08 kila Mwaka, ambapo kwa mara ya Kwanza yaliadhimishwa Mwaka 1911 Nchini Marekani
Awali akiwasilisha taarifa katika kongamano hilo Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Bernadetha Ntembeje alisema lengo la Maadhimisho ya Mwaka huu ni pamoja na kuongeza msukumo wa Ushiriki wa Wanawake katika uongozi na kwenye vyombo vya maamuzi
Alisema Jamii na Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamekuwa wakitoa taarifa katika vyombo husika kuhusu Vitendo vya ukatili vinavyofanywa katika makundi mbalimbali ikiwemo ukatili kwa Wanawake
Aliendelea kusema baadhi ya Wanaume wameelewa umuhimu wa usawa wa Kijinsia na kufanya Wanawake wengi kuingia kwenye shughuli za uzalishaji mali, Utawala, Maamuzi na kùsaidiana katika Majukumu ya kijamii
Katika kongamano hilo Wanawake hao walifanikiwa kujadili Suala la Malezi, Ukatili wa Kijinsia, Elimu ya Mahusiano, Mtazamo wa Jamii kuhusu Usawa wa Kijinsia, Ubunifu na Teknolojia rahisi ambazo ni chachu kuelekea Usawa wa Kijinsia
Nchini Tanzania maadhimisho haya yalianza Mwaka 1997 na Mwaka 2015 Serikali ilipitisha uamuzi wa maadhimisho haya yafanyike Kimkoa na Kitaifa na katika maadhimisho haya Mwaka huu Kauli mbiu ni "Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia; Chachu katika kuleta Usawa"
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa