Na mwandishi wetu.
Halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji leo may 7 kupitia meya wa halmashauri Mhe. Husseini Ruhava imesaini mkataba wa ujenzi wa mifereji ya maji taka na maji ya mvua kutokana na athari za mvua na mmonyoko wa ardhi katika mitaa ya halmashauri hiyo.
Mkataba huo ambao umeeleza kiasi kilichotengwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo ni kiasi cha shilingi za Kitanzania Billioni 1.65 ambapo kazi inatarajiwa kufanyika kwa mda wa miezi 12, mkataba huo umesainiwa katika ukumbi wa halmashauri baina ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na kampuni ya CHEIL Engineering Co. L.t.d kutoka jamhuri ya Korea ikishirikiana na kampuni ya kitanzania DOCH Limited .
Kiasi cha fedha hicho ni msaada kutoka Benki ya Dunia ikiwa inaratibiwa na mpango wa kuendeleza na ukuzaji wa miji na majiji kimkakati(TSCP),ambapo mradi huo unatariwa kuwa wa miaka 20 kuanzia mwaka 2019-2040.
Kabla ya kusaini mkataba huo meya wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji aliwakaribisha wageni hao , Wataalamu kutoka Mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma (KUWASA), Kamati ya madiwani ya fedha na uongozi, wakuu wa idara na vitengo pamoja na waandishi wa habari katika utiaji saini mkataba hiyo huku akisema ni mkataba utakaomaliza kero za wananchi katika mmomonyoko wa ardhi katika kata mbalimbali ambazo tayari zimeshapata athari ndogondogo za mmonyoko.
Akiwasilisha mmoja wa wajumbe wa kampuni hiyo ya CHEIL Co. L.t.d amesema kwa sasa watafanya upembuzi yakinifu kujua ni wapi ambapo maeneo hayo yameathirika ili waweze kufanya kazi na kuahidi kazi kufanyika katika hali ya ubora wakishirikiana na wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Kigoma(KUWASA) na wataalamu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo na Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dr. Peter Nsanya akiongea katika hafla hiyo amesema halmashauri iko tayari katika kutoa ushirikiano kwa kutoa wataalamu wa kushauri na kutoa maelekezo katika mradi huo na halmashauri itahakikisha inatoa mpango wa mambo gani yatakayofanyika katika mradi huo.
Wanufaika katika mradi huo ni wakazi wote wa manispaa ya Kigoma/Ujiji ambapo jumla ya kata 19 na mitaa 68 ya halmashauri hiyo inatarajiwa kunufaika na mradi huo wa kuendeleza na kukuza miji na majiji Tanzania.
Picha zaidi ingia www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa