Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji inaendelea na utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Wananchi kwa kutumia makusanyo (mapato) ya ndani
kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 Manispaa hiyo ilipanga kutumia fedha za Kitanzania zaidi ya Billion moja (Tsh 1, 049, 175,000/=) ikiwa ni fedha zitokanazo na mapato ya ndani katika miradi ya Maendeleo ili kuwanufaisha Wananchi walio wengi
Aidha zaidi ya asilimia themanini (80%) ya fedha hizo sawa na Tsh 835, 000, 263. 74/= zimeendelea kutekeleza ujenzi wa miradi ya maendeleo katika kata kumi na tisa (19) za Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na Ujenzi wa Ofisi za Kata ambazo awali hawakuwa na ofisi kwa majengo ya Serikali , Ujenzi huo unaendelea katika Kata ya Rubuga ukiwa umegharimu fedha za Tsh 45, 000, 000/= ambapo hadi sasa Ujenzi huo ukiwa hatua ya Usafi na kupaka rangi jengo
Ofisi zingine za Kata zinazojengwa ni pamoja na Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Buhanda unaoendelea ujenzi wa boma na upauaji ukiwa umekamilika na kiasi cha fedha Tsh 40,000,000/= kikiwa kimetolewa, Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Katubuka, na Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mwanga Kusini ukiwa unaendelea
Aidha Ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Machinjio kwa kutumia mapato ya ndani unaendelea ukiwa umefikia hatua ya umaliziaji (Finishing) kwa fedha za Kitanzania zaidi ya Million Sabini na Mbili ( Tsh 72,000,000/=) na kukamilika kwa zahanati hiyo kutasaidia upatikanaji wa huduma ya matibabu karibu na Wananchi wa eneo hilo ambapo kwa sasa wanalazimika kufuata Matibabu nje ya Kata yao
Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kutumia Mapato ya Ndani kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 iliendelea na Uzalishaji wa Miche bora na ya kisasa eneo la Katosho ambapo ilitumia kiasi cha fedha Tsh 21, 080, 000/- na miche hiyo kuwagawia kwa Wananchi bure
Hatua hii ya uendelezaji wa Miradi kwa Mapato ya ndani ni hatua kubwa na ya kupongeza viongozi mbalimbali wa Halmashauri , ikiwa ni pamoja na Wananchi kwa kuunga juhudi za ukusanyaji kodi na utunzaji wa miundombinu na miradi ya Maendeleo
Endelea kutembelea www.kigomaujijimc.go.tz na Mitandao yake ya Kijamii
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa