Na Mwandishi Wetu
Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Kilumbe Shabani Ng'enda Leo Desemba 21, 2023 amezindua Zahanati mpya iliyojengwa kwa mapato ya ndani Kata ya Machinjioni Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuanza kutoa huduma kwa Wananchi.
Akihutubia Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutoa fedha katika kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na Wananchi wa Manispaa hiyo.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita ilitoa kiasi cha fedha za Kitanzania Million Mia tano (Tsh 500, 000,000/=) kwa lengo la upanuzi Kituo cha afya cha Gungu, Million Mia tano (Tsh 500, 000, 000/=) Ujenzi wa Kituo cha afya cha Buhanda, Million Mia mbili (Tsh 200, 000,000/=) kukamilisha Ujenzi wa Zahanati ya Kamala ,Kibirizi na Kitongoni na Kiasi cha zaidi ya Billion Moja (Tsh 1, 300, 000, 000/=) kwa Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa unaoendelea Kata ya Kagera.
Aidha ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kutekeleza miradi kupitia Makusanyo yake ya ndani ambapo Zahanati imejengwa kwa fedha za Kitanzania zaidi ya Millioni Mia moja thelathini na nne (Tsh 134,000,000/=), Mapato ya ndani yakiwa ni zaidi ya Million mia moja na ishirini (Tsh 123,000,000/=) na Fedha kutoka Mfuko wa Jimbo Million kumi na Moja ( Tsh 11, 000, 000/=) na Vifaa tiba vikigharimu kiasi cha Million Hamsini (Tsh 50, 000, 000/=).
Akiongea Katika Mkutano huo Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli amesema Baraza la Madiwani limeendelea kutekeleza na kusimamia Miradi ya Maendeleo kupitia Mapato ya ndani kwa kujenga Ofisi za Kata, Uzalishaji Miche ya Michikichi ya Kisasa na Ujenzi wa Zahanati katika kata mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amesema kuzinduliwa kwa Zahanati hiyo kumefanya Manispaa hiyo kuwa na Zahanati tisa (09) huku akiahidi kusimamia nidhamu ya Watumishi kwa kutoa huduma bora na kuwataka Wanachi kutunza miundombinu iliyopo.
Zaidi endelea Kubofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa