Na Mwandishi Wetu
Waratibu wa elimu Kata na Walimu wa Mpango wa elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA) Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo March 26, 2023 wamehitimisha mafunzo ya siku tatu (03) yaliyokuwa na lengo la kujifunza namna ya ufundishaji elimu Jumuishi kwa Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu
Mafunzo hayo yalifunguliwa siku ya Ijumaa March 24, yakiongozwa na Wakufunzi kutoka Chuo cha Ualimu Patandi Arusha yakifadhiliwa na Shirika la UNICEF
Katika mafunzo hayo mikakati na mipango ya namna ya ufundishaji Wanafunzi wenye Umri miaka 8-13 na kwa vijana walio na umri 14-18 kupitia elimu ya MEMKWA kwa Wenye ulemavu na wenye mahitaji Maalumu yaliweza kujadiliwa
Walimu wa MEMKWA wamesisitizwa kuendelea kuwatambua Wanafunzi wenye ulemavu na wenye mahitaji Maalumu na kuhakikisha wanazingatia mbinu za ufundishaji ili kufikia malengo yaliyokusudiwa
Wametakiwa Kuzingatia elimu Jumuishi kwa kuhakikisha wenye ulemavu na wasio walemavu wanajifunza pamoja ili kuondoa dhana potofu kuhusu ulemavu na kuendelea kuwajengea stadi za maisha
Mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo Ubainishaji wa makundi mbalimbali ya watoto wenye mahitaji maalumu, afua stahiki kulingana na makundi ya watoto wenye mahitaji maalumu, Wanafunzi wenye ulemavu kushiriki shughuli za Kitaalamu na kijamii, na Uboreshaji na uimarishaji wa miundombinu rafiki kama Madarasa na vyoo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa