Na Mwandishi Wetu
Wazazi wa Kitanzania wametakiwa kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao juu ya hedhi salama na kuepukana na mitazamo hasi
yamesemwa hayo katika Mdahalo ulioandaliwa na Shirika la Bakaids wakishirikiana Shirika la Norwegian Church Aid(NCA) uliofanyikia Shule ya Sekondari Katubuka iliyopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji likihusisha Washiriki Wanafunzi kutoka Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza
Mgeni Rasmi wa Mdahalo huo na Afisa Elimu Taaluma Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Tabu Maalim amesema wazazi wa Wanafunzi wa kike wana wajibu wa kutenga bajeti kila mwezi kwa ajili ya kununua taulo za kike pindi wanapokuwa katika siku zao ikiwa ni pamoja na kuwajenga kiakili ili waweze kujiamini pindi wanapokuwa wakifanya kazi zingine ikiwemo Masomo katika kipindi hicho
Aidha Mgeni Rasmi huyo amewataka Wanafunzi wa kike kuendelea kujifunza elimu zaidi juu ya hedhi salama kwa kuzingatia usafi, kutumia taulo kwa usahihi na kuepukana na dhana potofu ili kuendelea kujifunza Masomo ya kitaaluma katika kipindi chote cha hedhi
Amewataka wadau mbalimbali, Asasi, na Mashirika kuendelea kutoa elimu ya hedhi salama na kutoa vifaa kama vile taulo, ujenzi wa vyumba vya kujisitiri mashuleni huku akisema Serikali itaendelea kutenga bajeti ya kuunga jitihada za hedhi salama katika taasisi za elimu
Mratibu wa afya ya uzazi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Pendo Samizi amewataka wanafunzi hao wa Shule za Msingi na Sekondari kuzingatia usafi kwa kuoga kila mara pindi wanapokuwa katika siku za hedhi huku akisema uvaaji wa taulo moja ya kike zaidi ya masaa manne ni hatari kwa afya
Ameendelea kusema athari za kutozingatia usafi wa mwili katika kipindi cha hedhi salama ni pamoja na Muwasho, halafu mbaya na kupata ugumba
Afisa elimu afya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Gunaguje Bukeye amesema kwa sasa Serikali imetoa mwongozo wa kujenga kwa vyumba vya kujisitiri kwa wanafunzi wa kike katika miundombinu yote ya Vyoo vinavyojengwa kwa Shule zote huku akiendelea kusema kuwa Serikali inatenga bajeti ya afya katika fedha za uendeshaji shule jambo linalofanya Walimu Wakuu Mashuleni kununua vifaa tiba vya huduma ya kwanza ikiwemo taulo za kike
Afisa Mradi wa Shirika la Bakaids Ndugu. Juma Bewa amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa elimu ya hedhi salama ili kuhakikisha Wanafunzi walio wengi kuepuka vizuizi, unyanyasaji na dhana potofu katika kipindi chote cha Masomo hata anapokuwa katika jamii
Mchungaji wa Kanisa la CCT na Mratibu wa Waking the Giant Nchini Tanzania Mch. Modest Pesha akishiriki Mdahalo huo kwa njia ya mtandao amewataka wazazi wa jinsi ya kiume kuzungumza na watoto wao na kuwa msitari wa mbele katika kuwahudumia taulo za kike katika kipindi chote na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya usafi majumbani ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafu katika kipindi cha hedhi
Awali wakichangia katika Mdahalo huo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kandaga Wilayani Uvinza Vanesa Omary na na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Katubuka Anna John wamesema wanafunzi wengi wa kike kila mwezi kukosa Masomo kuanzia siku Sita (6) hadi nane (8) ambapo hukumbana na athari za kushuka kitaaluma, kunyanyaswa na Wanafunzi wa kiume na kuwashusha thamani huku wakiitaka Serikali na vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu juu ya hedhi salama kwa makundi yote ndani ya jamii
Maadhimisho haya yamewashirikisha wawakilishi wa Wanafunzi Wilaya ya Uvinza na Manispaa ya Kigoma, Wataalamu wa Afya, Viongozi wa Dini, Wataalamu wa Elimu, wazazi na Vyombo vya habari na maadhimisho haya Kitaifa Mwaka huu yanafanyikia Mkoani Kigoma Uwanja wa Mwanga Community centre kesho May 28, 2022
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa