Na Mwandishi Wetu
Wajumbe wa Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Kigoma Ujiji wakiongozwa na Meya wamesikitishwa na mwenendo na kasi ya ujenzi wa miradi ya TACTICS inayoendelea kutekelezwa.
Viongozi hao wameoneshwa kusikitishwa walipofanya Ziara Leo Januari 06, 2024 katika maeneo ya miradi huku wakioneshwa kutoridhishwa na kasi ya ujenzi.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Meya huyo Mhe. Baraka Naibuha Lupoli amesema Mkandarasi wa ujenzi wa soko la Mwanga na Mwalo wa Katonga kutoka kampuni ya ujenzi ya ASABHI CONTRACTOT LIMITED kwa kushirikiana na PIONEER wako nyuma ya Mkataba kwa mda wa miezi minne tangu kusainiwa kwa mkataba.
Huku mradi huo wenye gharama ya fedha za Kitanzania zaidi ya Billioni kumi na Sita (Tsh 16, 495, 359, 710. 275/=) inatekelezwa kwa mda wa miezi kumi na mbili (12) kuanzia Novemba 15, 2024 hadi Novemba 14, 2025 ambapo utakuwa umekamilika.
Aidha Meya akiwa katika eneo la ujenzi wa daraja la Mto Ruiche inayotekelezwa na kampuni ya ujenzi ya CRJE amesema Mradi huo kwa mjibu wa Mkataba unatarajiwa kukabidhiwa February 20, Mwaka huu huku Hadi sasa ukiwa umefia asilimia arobaini na mbili (42%) ya utekelezaji.
Amesema kampuni Zote zimeonesha kuchelewa kutekelezwa kwa mradi huku akionesha mashaka na kampuni hizo na akisema Halmashauri itafuata taratibu za kuvunja Mkataba.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa