Na Mwandishi Wetu
Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo April 22, 2024 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inavyotekelezwa katika Kata za Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Ziara hiyo imefanyika ikiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Baraka Naibuha Lupoli huku Wajumbe wakipongeza namna ambavyo Ofisi ya Mkurugenzi imeendelea kusimamia miradi ya maendeleo.
Ziara hiyo imefanyika kukagua na kutembelea Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari eneo la Burega Kata ya Buzebazeba kwa gharama ya Tsh 603, 890,563.00/=, na Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kata ya Kipampa kwa gharama ya Tsh 603, 890,563.00/= ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu.
Miradi mingine iliyotembelewa ni Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kasimbu kwa gharama ya fedha Tsh 63,676,400/=, na Ujenzi wa Zahanati ya Rubuga kwa gharama ya fedha Tsh 130,000,000/= ikiwa ni fedha kutoka Mapato ya ndani.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa