Na Mwandishi wetu
Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe.Baraka Lupoli jana Januari 20,2021 alikutana na machinga wa soko la Kibirizi na kutatua changamoto zao huku akitembelea waathirika wa maji ya Mvua iliyonyesha katika Manispaa hiyo
Meya huyo alifanya ziara hiyo akiwa na Waheshimiwa Madiwani ambao pia ni Wajumbe wa Kamati ya fedha na Uongozi huku akizungukia miundombinu ya barabara na mitalo iliyovunjika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha alfajiri ya kuamkia siku ya Jumanne Januari 19,2021
Akiwa katika ziara hiyo iliyoanzia katika mwalo wa Kibirizi wajasiliamali na machinga wauza nguo wa soko la Kibirizi walimfikishia kilio chao cha kukosa sehemu ya kuuzia bidhaa zao hizo kutokana na eneo waliokuwa wakiuzia awali kujaa maji ya mvua na kusababisha adha na kushindwa kufanya biashara zao na kutojiingizia kipato kutokana na changamoto hiyo
Naye meya huyo akiwa katika soko hilo aliwataka machinga hao kuendelea na biashara zao huku akiwaonesha eneo la kuuzia bidhaa zao katika soko la kibirizi licha ya kuwa na mwingiliano wa bidhaa tofauti tofauti kukaa sehemu moja huku akiwataka kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho eneo lililojaa maji litakuwa likifanyiwa ukarabati na kurudi eneo lao mara tu litakapokuwa limekamilika
Mmoja ya wamachinga wa nguo katika soko hilo Astala Rajabu Mrisho alimshukuru na kumpongeza Meya huyo kwa kusikia kilio chao huku akimtaka kushughulikia eneo hilo lililojaa maji kwa wakati na kuendelea kutatua changamoto za wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Aidha katika ziara hiyo iliyofanyika Meya wa Manispaa hiyo alifanya kikao na wasafirishaji wa nje (Expoters) wa mazao ya uvuvi kwa kusikiliza changamoto zao huku akitembelea wananchi walioathirika na kuharibikiwa vitu kutokana na mvua kubwa iliyonjesha na kuingia katika makazi yao na kutembelea miundombinu ya barabara na mitaro iliyovunjika
Kata alizotembelea kutokana na miundombinu iliyoharibika na maji ya Mvua ni kata ya Kigoma, Mwanga kaskazini, Mwanga Kusini, Buhanda ,Katubuka, Burega, Gungu, na kata ya Rubuga.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa