Afisa biashara Festo Nashoni akieleza namna stika itakavyokuwa inafanya kazi na kukomboa mda kwa madereva tofauti na ushuru wa awali.
wamiliki wa bajaji na bodaboda katika kikao na Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Na mwandishi wetu.
Meya wa manispaa ya Kigoma/Ujiji Hussein Ruhava jana January 18, amefanya kikao na wamiliki wa bajaji na bodaboda katika ukumbi wa manispaa na kutokana na malalamiko aliyoyapokea ofsini kwake.
Meya huyo akifungua kikao na wamiliki hao mara baada ya kukaribishwa na Afisa biashara wa manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa niaba ya Mkurugenzi Ndugu Festo Nashoni alisema ofsi yake ilipokea malalamiko namna dereva wa bajaji wanavyopoteza mda wakiwa kazini pindi wanapotozwa ushuru wa siku kutokana na kusimama kwa mawala pindi wanapokata risti.
Aliendelea kusema katika kutatua changamoto hiyo aliituma timu ya wataalamu katika kufatilia namna gani wanaweza kutatua changamoto hiyo na kuhakikisha mapato hayapotei, jambo lililofanya wataalamu hao kupitia ofsi ya Mkurugenzi kuja na wazo la kukata stika kwa mwezi kwa lengo la kuleta ufanisi katika kuongeza mapato ya halmashauri na kuwanufaisha madereva na wamiliki wa vyombo hivyo.
Aliendelea kusema “utaratibu huo wa stika kwa kila mwezi tumeanza nao kuutumia January 2 mwaka huu kwa wamiliki wa bajaji na bodaboda kulipia shilingi za kitanzania elfu kumi na tano (15000/=) na tutahakikisha tunadhibiti watu wote wanalipia stika hizo jambo litakaloondoa usumbufu kwenu ninyi wamiliki na madereva wenu”.
Nao wamiliki wa vyombo hivyo waliweza kueleza changamoto zinazowakabili , mmoja wa wamiliki na kiongozi wao Ndugu Jumanne Gange alisema wanazo changamoto nyingi pindi wanapokuwa barabarani kwa kudhibitiwa na Askari wa ulinzi na usalama barabarani katika maeneo wanayopakilia abiria jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo yao na kusema kiwango cha ushuru kilichowekwa kwa mwezi ni kikubwa sana kwani sio mara zote madereva wanakuwa barabarani wakifanya kazi hiyo na mara nyingi bajaji hizo hupelekwa katika matengenezo(service).
Naye katibu wa wamiliki wa bajaji na bodaboda maarufu kwa jina la Kibopa alisema hakubaliani na ushuru huo wa Tsh 15000/= kwa mwezi na kutaka ushuru uendelee kutozwa wa Tsh 500/= kwa siku jambo lilioleta majadiliano na mvutano mkubwa katika kikao hicho.
Akitoa ufafanuzi katibu wa kikao hicho na Afisa biashara aliwataka wamiliki na viongozi hao kukubaliana na utaratibu uliowekwa wa kutumia stika kwa mwezi kwani tayari walikuwa wameshakutana na viongozi wao na kuweza kukubaliana na viongozi hao kulidhia utaratibu wa stika jambo linaloleta mvutano kwa viongozi nhao kutokuliana katika kikao hicho.
Naye mmoja wa wajumbe wa kikao hicho mmiliki na dereva aliyejulikana kwa jina moja Mussa alipongeza jitihada za halmashauri katika kujali na kuweka mzingira mazuri japo alisema kiwango hicho ni kikubwa na kuomba kupunguziwa ushuru huo.
Naye meya wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma ujiji alitoa tamko kwamba kuanzia mwezi February wamiliki wa vyombo hivyo watalipia Tsh 13000/=kama msimamo wa halmshauri na kusema kiwango hicho kimezingatia hata siku za matengenezo (service).
Alihitimisha kikao hicho kwa kuwashukuru na kuwapongeza wamiliki hao na kusema wataendelea kukaa pamoja katika kuhakikisha hata baadhi ya changamoto zinatatuliwa na kuwataka kutii kanuni na sheria za nchi katika uendeshaji wa vyombo hivyo vya moto.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa