Na Mwandishi wetu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr. Saimon Chacha leo june 2, amefanya ziara katika shule na vyuo vilivyo anza masomo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kukagua kama hatua za kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 zinachukuliwa kwa walimu na wanafunzi
Mganga mkuu huyo akiwa katika ziara hiyo amesema kwa Mkoa wa Kigoma hakuna Mgonjwa wa Covid-19 huku akiwataka wanafunzi na walimu kutokuwa na hofu katika suala la ujifunzaji na ufundishaji bali waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo
Akiwa katika chuo cha Uuguzi Maweni amepongeza uongozi wa chuo hicho kwa hatua walizozichukua katika kuhakikisha kila mtu anayeingia na kutoka anahakikisha anapimwa joto la mwili wake na kunawa huku katika madarasa yao wakikaa kwa hatua ya mita moja moja ili kuepukana na msongamano darasani
Aidha Mganga Mkuu ameendelea kuwasisitiza wanafunzi na wanachuo kuepuka suala la kukumbatiana na kubusiana kutokana na wanafunzi na wanavyuo kuwa na mazoea hayo mara wanapokutana mara kwa mara kama marafiki , kunawa maji safi yanayotiririka kwa sabuni na kuvaa barakoa kila mara wanapokuwa darasani
Naye Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Kigoma Ndugu. Omari Mkombole amewataka walimu wanapokuwa wakifundisha darasani kuingiza na mada mtambuka kila mara namna ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 huku wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Kigoma na Buronge wakiaswa kutumia mda mfupi uliobaki kuelekea mitihani kuutumia kwa usahihi ili kuweza kufanya vizuri katika ufaulu wa mitihani
Kaimu mkuu wa chuo cha Uhasibu (TIA) Tawi la Kigoma Ndugu. Charles Merengo amesema tayari wanachuo wa chuo hicho wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 na wanafunzi wote na walimu hupimwa joto la mwili kila wanapoingia katika chuo hicho , ameendelea kusema kwa sasa ratiba ya masomo imerekebishwa awali ratiba iliishia saa nane na kwa sasa ratiba mwisho saa kumi na mbili jioni kutokana na kupunguza idadi ya wanafunzi darasani kwa wakati mmoja
Mwanachuo wa chuo cha Uuguzi Maweni Bi. Jackie Kazinga amesema wao kama wanachuo wanachukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 kwa kunawa maji safi yanayotiririka, kuvaa barakoa na kukaa darasani kwa umbali unao takiwa
Pia mwanachuo wa Chuo cha Uhasibu (TIA) Ndugu. Hassan Kigongo amesema tayari masomo yameanza chuoni hapo na wanachukua tahadhari zote katika ujifunzaji kwa kuhakikisha wanachukua tahadhari ya kujikinga na Ugonjwa wa Covid-19 na tabia za kukumbatiana na kubusiana kama zilivyokuwa awali
Mei 21,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli alisema vyuo vikuu vyote vitarejea katika hali yake ya kawaida ya kuendelea na masomo kuanzia June mosi baada ya kujiridhisha kutokana na maambukizi ya virusi vya Ugonjwa wa Covid-19 kupungua Nchini Tanzania
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa