Na Mwandishi wetu
Wahudumu wa afya ngazi ya vituo Manispaa ya Kigoma/Ujiji leo September 29, 2021 wametakiwa kuendelea kutoa elimu ya chanjo ya Uviko-19 katika maeneo yao ya kazi
Wito huo umetolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr. Saimon Chacha alipokuwa Mgeni Rasmi katika semina ya Mpango harakishi na shirikishi wa Uchanjaji ya Chanjo ya Uviko-19 kwa wahudumu hao wa afya iliyofanyika katika Ukumbi wa chuo cha Waganga Maweni
Katika semina hiyo Mganga Mkuu huyo amewataka watumishi hao wa afya kuwa mstari wa mbele katika uchanjaji wa chanjo ya Uviko-19 na kuhakikisha jamii inapata taarifa zilizo sahihi juu ya chanjo hiyo inayoendelea kutolewa Nchini
Aidha Mganga Mkuu huyo amesema Mpango harakishi na shirikishi utaweza kuwafanya Wananchi kupata elimu ya uchanjaji kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali , Watu maarufu , na Viongozi wa dini kushiriki zoezi la kutoa elimu ya Uchanjaji na kufanya asilimia sitini (60%) ya wakazi wa Mkoa wa Kigoma wanapata chanjo ya kujikinga na Uviko-19
Akitoa takwimu mganga Mkuu huyo amesema Mpango huo utaleta matokeo chanya na kuwa na jamii yenye watu wenye afya bora ambapo kwa mkoa wa Kigoma utakuwa na vituo mia mbili hamsini na saba (257) kutoka vituo ishirini na nne(24) vya awali huku Manispaa ya Kigoma/Ujiji ikiwa na vituo kumi na saba (17) kutoka vituo vitatu (03) vya awali
Ameendelea kusema ongezeko la vituo hivyo litaleta tija kwa wananchi kujitokeza kuchanja kwa wingi kutokana na vituo vingi kuwa karibu na maeneo ya makazi na kupunguza kusafiri mda mrefu kwa kufuata chanjo hiyo
Amehitimisha kwa kueleza njia zingine zitakazotumika kuwafikia wananchi katika uchanjaji ikiwa ni pamoja na kuwa na huduma tembezi ya kuwafikia wananchi moja kwa moja katika makazi yao na kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa elimu ya Uviko-19
Awali Mratibu wa chanjo ya Chanjo Manispaa ya Kigoma/Ujiji akimkaribisha mgeni rasmi Ndugu. Waziri Shabani alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa na uwezo watoa huduma wa afya ngazi ya vituo mpango harakishi na Shirikishi wa Uchanjaji Chanjo ya Uviko-19 ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wachanjaji kwa lengo la kuwa na jamii imara na yenye afya njema
#tusifikehuko #ujanjakuchanja #jikingewakingewengine #jikingewakingewenginecoronainazuilika #jikingewakingewenginekaziiendelee #elimuyaafyakwaumma
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa