Na Mwandishi Wetu
Wananchi na wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Desemba 6, 2022 wamejitokeza kufanya usafi na utoaji msaada wa mahitaji kwa Wagonjwa katika kituo cha afya cha Ujiji ikiwa ni mwendelezo wa wiki ya Sherehe ya Miaka sitini na Moja (61) tangu Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika ilipojipatia Uhuru wake Desemba 9, 1961
Wananchi hao wamejitokeza wakiongozwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Maximillian Cyrillo ambapo amewapongeza Wananchi hao kwa kushiriki sherehe za maadhimisho Wiki ya uhuru wa miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara huku akisema maadhimisho hayo kwa Wilaya ya Kigoma yameanza Desemba 02, 2022 kwa kufanya shughuli mbalimbali za Kijamii
Amesema Shughuli za Kijamii ambazo tayari zimetekelezwa ni pamoja Usafi masokoni, Upandaji wa Miti na miche ya kisasa ya Michikichi, na Usafi katika vituo vya afya
Ameendelea kusema Kesho Desemba 07, 2022 shughuli ya mazoezi ya Viungo ya mchakamchaka (Jogging) yataanzia Stesheni ya Kigoma Saa kumi na mbili (12:00) Asubuhi na kuhitimishwa Uwanja wa Mwanga Community Centre kwa zoezi la utoaji damu
Aidha amesema Desemba 8, sherehe hizo zitaendelea katika Uwanja wa Lake Tanganyika kwa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa Miguu, riadha, uvutaji kamba, na kukimbiza kuku kuanzia majira ya Saa moja asubuhi
Amehitimisha kwa kusema kilele cha maadhimisho hayo kitahitimishwa katika Ukumbi wa nnsf Kigoma kwa kujadiliana maendeleo ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara awali ikiitwa Tanganyika
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni " Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu ".
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa