Na mwandishi wetu
Uzinduzi wa ugawaji miche ya michikichi ya kisasa kwa wakulima umefanyika leo Novemba 25, kwa kugawa bure miche elfu kumi na moja (11,000) kwa wanufaika na wakulima mia moja na hamsini huku zoezi la upandaji wa miche hiyo kando ya barabara za mji ukifanyika
Katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mwailwa Pangani amewataka wakulima kuhakikisha wanaitunza miche hiyo na kuihudumia mashambani ili kuendeleza ubora wa uzalishaji wa mawese kwa kiwango cha juu na kuepukana na uagizaji wa mafuta ya mawese nje ya Nchi
Aidha mkurugenzi huyo amezitaka kaya na familia ambazo miche hiyo imependwa na itapandwa kando ya barabara za mji kuhakikisha miche hiyo inasitawi kutokana na gharama ya uzalishaji kuwa kubwa na sera iliyopo kuhakikisha Manispaa ya Kigoma/Ujiji inakuwa ya kijani kwa kustawisha zao hilo
Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa kilimo Kihinga (TARI) Ndugu. Kuzenza Madili Amewataka wakulima kuhakikisha wanatunza miche hiyo ili kufikia lengo la uzalishaji wa mawese kwa kiwango cha juu huku akiwataka Maafisa Ugani kuwafatilia na kuwapa ushauri wakulima katika ukuzaji wa zao hilo
Naye Kaimu Mkuu wa idara ya Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Haruna Mtandanyi amesema Manispaa hiyo ina lengo la Kuzalisha miche Millioni Moja (1,000,000) ambapo kwa sasa tayari Miche Elfu thelathini (30,000) imeshazalishwa na utengaji wa bajeti ya uzalishaji wa miche iliyobaki umefanyika
Ameendelea kusema miche hiyo itagawiwa kwa awamu mbili ambapo kwa sasa wanufaika wengine ni pamoja na Taasisi tano (05) za serikali na barabara tatu(03) za mji za kiwango cha lami huku mwezi Februali 2021, ugawaji awamu ya pili miche elfu kumi na tisa(19,000) utafanyika na wakulima mia tatu na ishirini(320), taasisi tatu(03) na barabara nne (04) za lami za mji zikipandwa miche hiyo kando ya barabara
Bi. Shani Sasilo Mkulima wa bonde la Mto Ruiche ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuja na mkakati wa uzalishaji wa mafuta ya mawese kwa kiwango cha juu na kulifanya zao la michikichi kuwa la kimkakati huku akisem mpango huo wa Serikali utafanya wakulima kujikomboa kwa kupata mafuta yaliyobora kutokana na miche hiyo
Katika Hotuba ya Rais Dr. John Pombe Magufuli akifungua Bunge la kumi na mbili (12) alilitaja zao la Michikichi kama zao la kimkakati ambalo litasaidia uzalishaji wa mafuta ya mawese kwa kiwango kikubwa ,miche hiyo ya kisasa ikiwa na uwezo wa kuzalisha Tani 4.5 hadi Tani 5 kwa hekta kwa mwaka ambalo litapelekea kuepuka uagizaji wa mafuta hayo Nchini Malaysia na Nchini Burundi ambapo zaidi ya fedha za Kitanzania Billion 445 hutumika kila mwaka kuingiza mafuta hayo
picha na video zaidi ingia maktaba ya picha www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa