Na Mwandishi Wetu
Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Manispaa ya Kigoma Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amewataka Wananchi kujitokeza kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa katika Uchaguzi utakaofanyika Siku ya Jumatano Novemba 27, Mwaka huu.
Ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha #sikumpya kinachorushwa kupitia @mainfm 91.7 ambapo pia amewataka kujitokeza kwa wingi katika kipindi cha Kampeni kuwasiliza Wagombea kupitia mikutano ya Kampeni itakayofanyika kupitia Vyama vya Siasa ili kufanya maamuzi yaliyosahihi katika Uchaguzi.
Amesema maandalizi ya Uchaguzi kwa Kigoma Mjini yamekamilika kwa kiasi kikubwa na kwa mjibu wa ratiba Kampeni zinatarajia kuanza Novemba 20-26.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa