Na Mwandishi Wetu
Mkataba wa kuanza kwa ujenzi wa Soko la Mwanga na Soko la mazao ya uvuvi Katonga hivi karibuni unatarajiwa kusainiwa ili kuanza kwa ujenzi wa masoko hayo kisasa.
Hayo yamebainishwa Jana Oktoba 16,2024 katika kikao cha mapitio ya miradi ya Uendelezaji wa Miji na Majiji Kimkakati Nchini Tanzania (TACTICS) kilichofanyika baina ya Wakuu wa idara na vitengo wa Manispaa na Wataalamu kutoka Kampuni ya ujenzi ya Saba Engineering Limited.
Katika kikao hicho Wataalamu hao walipata fursa ya kupitia Michoro ya Masoko hayo yote mawili.
Miradi hii inatekelezwa Chini ya ufadhili wa benki ya dunia (WB) ambapo miradi ya Awamu ya kwanza inaendelea kutekelezwa ikihusisha
Ujenzi wa Barabara ya Wafipa-Kagera yenye urefu wa Km 2.434, Daraja la Mto Ruiche, Ujenzi wa barabara ya Bangwe-Burega- Ujiji yenye urefu wa Km 7.1, na Ujenzi wa mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua katika maeneo ya Bangwe, Burega, Rutale, Mlole , Bushabani, Mji mwema, na Katonyanga yenye urefu Km 5.288.
Mkataba wa kuanza kwa ujenzi unatarajia kusainiwa hivi karibuni ukihusisha miradi ya Awamu ya pili ambayo ni Ujenzi wa Kisasa soko la Mwanga na Ujenzi wa Kisasa wa Soko la mazao ya Uvuvi Katonga.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa