Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma Ujiji imefanya Kikao na Wafanyabiashara wa Soko la Masanga kwa lengo la kujadiliana namna ya kutatua Changamoto zinazowakabili Wafanyabiashara hao.
Kikao hicho kimefanyika Leo May 03, 2024 huku wafanyabiashara wakitoa mawazo na mapendekezo katika kuboresha miundombinu na mazingira ya kibiashara katika soko hilo.
Akiongea na Wafanyabiashara Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amesema Manispaa imeendelea kufanya uboreshaji kwa kuhakikisha soko linakuwa na miundombinu rafiki ikiwemo upatikaji wa Maji, Umeme pamoja na ujenzi wa shedi za Wafanyabiashara wanaotumia vizimba.
Amesema lengo la Manispaa ni kuhakisha soko hilo linakuwa ni kivutio kwa Wafanyabiashara na Wateja katika kupata bidhaa mbalimbali.
Amewataka Wafanyabiashara kuendelea kutoa kodi na tozo za Manispaa huku akisema Halmashauri itaendelea kuboresha Mazingira ya Wafanyabiashara kupitia mapato ya ndani.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Soko la Masanga Ndugu. Joram Kinyuko ameipongeza Halmashauri kwa jitihada zinazoendelea katika kuhakikisha soko hilo linakuwa rafiki kwa Wafanyabiashara na Wateja wa bidhaa mbalimbali.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa