Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba Leo May 15, 2025 ametembelea miradi inayotekelezwa kupitia Mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali Kuu.
Amefanya ziara hiyo akiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo ambapo ametembelea Ujenzi wa Jengo la Mionzi na Jengo la Maabara katika Hospitali ya Manispaa iliyopo Kata ya Kagera, Ujenzi wa Bweni moja la Wanafunzi kwa gharama ya Tsh 680,000,000/= na Matundu ya vyoo Tisa (09) Kwa gharama ya Tsh 18,000,000/= Shule ya Sekondari Wakulima Kupitia Mradi wa Wezesha Binti.
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Shule ya Sekondari Buronge kwa gharama ya Tsh 136, 000,000/=, Ujenzi wa Chumba cha Kujifungulia Zahanati ya Businde kwa gharama ya Tsh 8,000,000/= fedha kutoka Mfuko wa Jimbo na Ujenzi wa Matundu ya vyoo 7 Shule ya Msingi Businde kwa gharama ya Tsh 15, 400,000/= fedha kutoka Mapato ya ndani.
Mkurugenzi huyo amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo ikamilike kwa wakati na kuleta tija kwa Wananchi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa