Mkurugenzi mpya wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Ndugu. Mwailwa S. Pangani ameongea leo August 31, na watumishi wote wa ofsi kuu katika ukumbi wa halmashauri huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa waledi ikiwa ni pamoja na kuheshimu serikali ya tano iliyoko madarakani.
Ameyasema hayo katika mkutano wa watumishi akiwa na wakuu wa idara wakiongozwa chini ya Afisa Utumishi Ndugu. Berneth Ninalwo ambapo mkurugenzi huyo amesema lengo kuu ni kufahamiana na watumishi wote na kuzungumzia namna ya utendaji kazi katika halmashauri.
Mkurugenzi huyo ameendelea kuwataka watumishi kutoa ushirikiano katika shuguli zinazofanyika kila siku na kuzifanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuweza kuondokana na tatizo la kupata hati chafu kwa miaka mitatu mfululizo jambo ambalo linatia aibu kwa halmashauri zingine nchini.
Akizungumzia changamoto inayozungumzwa ya hati chafu ikiwa ni mwingiliano wa wanasiasa na wataalamu amesema tatizo sio wanasiasa tu lakini pia wataalamu wamekuwa ni tatizo kubwa kutokana na namna wanavyofanya kazi kwa uzembe na kufika kazini kwa mda wanavyotaka jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya manispaa hiyo, mkurugenzi huyo anasema “wanasiasa sio tatizo sana hata ninyi wataalamu mnasababisha, kwani suala la mapato wanasiasa ndio wanaokusanya?, hivyo nawaomba tufanya kazi kwa weredi”.
Akiendelea kuongea amewataka watumishi hao kuitii serikali iliyoko madarakani hata kama mtumishi atakuwa na itikadi tofauti kwa kuwataka watumishi kuwahi kazini kwa wakati na kuondoka kwa wakati kutokana na sheria na kanuni za utumishi wa umma zinavyotaka ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi ya heshima kwa kila mtumishi ili kuleta ufanisi mzuri katika utendaji kazi.
Ameendelea kuwataka watumishi hao inapotokea tatizo la aina yeyote kufika ofsini na kutafuta namna ya kufanya utatuzi wa matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuacha majungu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Naye afisa utumishi Ndugu. Berneth Ninalwo katika mkutano huo amempongeza Mkurugenzi huyo kwa hatua nzuri aliyoanza nayo katika kuongea na watumishi wote kwa lengo la kuleta ufanisi katika kazi na afisa utumishi huyo amemuahidi mkurugenzi kutoa ushirikiano kwa watumishi wote waliopo chini yake na kusema kwa yale yote aliyoyaagiza yatasimamiwa ili kuleta ufanisi katika kazi.
Naye Ndugu Shabani mashaka na Meleji Mollel watumishi wa halmashauri hiyo wameweza kutoa pongezi kwa mkurugenzi huyo kwa kuteuliwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtaka mkurugenzi huyo kushugulikia masilahi ya wafanyakazi, upotevu wa mapato, na masuala ya hati chafu jambo ambalo linaichafua halmashauri hiyo.
Naye mkurugenzi huyo amehitimisha kwa kuwashukuru watumishi wote hao kwa kuhudhulia katika mkutano huo na kusema maoni yaliyototewa atayafanyika kazi kadri ya uwezo wake na kuwataka kuwa na upendano pamoja na ushirikiano katika majukumu ya kila siku ili manispaa iweze kusonga mbele.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa