Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amepongeza Wataalamu, Wakulima, Wafugaji na Wajasiriamali walioandaa na kushiriki uandaaji wa Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane Nane ) kanda ya Magharibi Mkoani Tabora Mwaka 2024.
Pongezi hizo amezitoa Leo August 13, 2024 alipokuwa akikabidhiwa tuzo na vyeti vya ushindi kwa nafasi kwanza (01) katika kundi la Halmashauri za Mkoa wa Kigoma na Tabora, na kuwa mshindi wa kwanza (01)wa jumla iliyojumuisha makundi ya Mashirika, Taasisiza Fedha, Taasisi za Utafiti, Mawakala na makampuni ya mbegu, Kampuni za Mawasiliano na Majeshi kanda ya magharibi.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka Wataalamu hao kuendelea kuwasaidia na kutatua changamoto za Wakulima, Wafugaji na Wajasiriamali katika maeneo yao kwa lengo la kukuza uchumi wa Mtù mmoja mmoja, familia, Manispaa na Taifa.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @mabuba_fkm @ortamisemi @wizara_ya_kilimo @mifugonauvuvi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa