Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mwailwa Pangani juzi August 2 alifanya ziara katika shule sita zilizopo katika manispaa hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hizo zinazojengwa kwa fedha za serikali kuu na baadhi ya wafadhili.
Ziara hiyo alifanyika na mkurugenzi huyo akiwa na wakuu wa idara na vitengo katika kuhakikisha fedha zilizoingizwa katika akaunti za shule zinatumika ipasavyo katika usimamizi shirikishi wa kamati ya shule na ofisi ya mwalimu mkuu husika ikiwa ni kuleta uwazi katika suala la uwajibikaji na usimamizi wa mali za umma.
Baada ya kuwasili katika shule ya msingi Bushabani mkurugenzi huyo alisomewa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vitatu na ofisi moja itakayogharimu jumla ya fedha za kitanzania Shilingi Milion 37,500,000/= ambapo ujenzi unaendelea katika hatua ya mwisho ambapo shule hiyo inavifaa vyote vya ujenzi na tayari fundi inayeendelea na ujenzi ameshalipwa fedha zake na kubaki na akiba ya milioni 10,043,400/= jambo ambalo mkurugenzi aliweza kulisifia
Katika ziara hiyo mkurugenzi huyo aliweza kuwasili katika shule ya sekondari Buronge ambapo alisomewa taarifa na mkuu wa shule hiyo kwa kueleza fedha iliyopokelewa kutoka katika miradi ya EP4R fedha za Kitanzania kiasi cha million 146,600,000/= kwa ujenzi wa wa vyumba viwili vya madarasa kwa Shilingi million 40,000,000/=, vyoo matundu sita kwa bajeti ya shilingi million 6,600,000/= na ujenzi wa bwalo moja kwa shilingi million 100,000,000/=
Mkuu wa shule hiyo aliendelea kueleza ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo upo katika hatua ya upakaji rangi na ukamilishaji wa madirisha huku katika bwalo ikiwa ni hatua ya kuezeka na kuwekewa fremu za madirisha na venti zake
Mkuu huyo aliendelea kueleza maendeleo ya shule hiyo kitaalauma kwa kueleza shule imeendelea kuboresha matokeo ya kidato cha nne ambapo kwa mwaka 2017 shule ilipokea zawadi kutoka wizara ya elimu, sayansi na teknolojia kwa kuwa miongoni mwa shule zilizoboresha matokeo
Ambapo pia alieleza matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2019 S hule ilikuwa na watahiniwa 142 wote wakiwa niwakutwa ambapo shule ilifaulisha kwa asilimia mia moja kwa daraja I wanafunzi 10, daraja II wanafunzi 76 walifaulu, daraja la III wanafunzi 45 walifaulu , daraja IV wakifauru wanafunzi 6 bila kuwa na wanafunzi waliopata daraja 0.
Baada ya hapo ziara iliendelea katika shule ya msingi Airport na Businde ambapo ujenzi umekuwa ukiendelea kwa kusuasua kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika uongozi wa shule hizo kuanzia kamati za shule jambo ambalo Mkurugenzi huyo aliahidi kulifatilia na kuachia vyombo vya Takukuru katika kuendelea na uchunguzi.
Ziara iliyofanyika shule zingine zilizotembelewa ni pamoja na shule ya msingi Rutale, shule ya msingi Kilimahewa na shule ya msingi Burega ambapo mkurugenzi wa halmashauri hiyo amewaasa wakuu wa shule na walimu wakuu kusimamia uimara na ubora wa majengo hayo yanayojengwa ili kuweza kuleta mazingira mazuri ya ujifunzaji na ufundishaji kwa walimu na wanafunzi kwa lengo la kuinua elimu na kufikia uchumi wa kati katika uwekezaji wa kielimu.
Aidha wakuu wa shule na walimu wakuu wakishirikiana na kamati za shule walipongeza ziara aliyoifanya mkurugenzi huyo akiwa na wataalamu wake kwani italeta tija njema katika usimamizi wa miundombinu na kumhakikishia kwamba miundombinu hiyo itakuwa chachu ya kukuza elimu na kuinua matokeo kwa wanafunzi mashueni.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa