Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Mwailwa Pangani jana februali 26, alitembelea miradi ya ujenzi inayoendelea kujengwa katika halmashauri hiyo
Mkurugenzi huyo alitembelea ujenzi wa miradi unaoendelea akiwa na baadhi ya wataalamu kutoka Ofisi yake huku baadhi ya miradi ni viporo vya mda mrefu tangu ianze kujengwa katika halmashauri ,
Akiwa katika shule ya Msingi Ujiji Mkurugenzi alipewa na taarifa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kuwa ukamilishaji wa nyumba mbili za walimu ambazo zilianza kujengwa tangu mwaka 2006 katika shule hiyo unaendelea na umefika hatua ya upauaji na ndani ya mwezi mmoja nyumba hizo mbili zitakuwa zimekamilika
Aidha Mwalimu mkuu wa Shule hiyo alimwelezea Mkurugenzi uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo kuwa majengo ya madarasa yale ni ya mda mrefu hali inayofanya baadhi ya madarasa kuanza kuvunjika huku mkurugenzi akiahidi kutatua hali hiyo kwa kuanza na ukarabati wa madarasa hayo
Akiwa katika eneo ambalo Zahanati ya Buronge inajengwa Mkurugenzi huyo alipewa taarifa na Mganga Mkuu wa Manispaa Dr.Siwale kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza tangu mwaka 2017 na unasimamiwa na Ofisi ya Kata ya Kibirizi, na upauaji umekamilika huku wakiendelea na usafi wa majengo hayo na kusema tayari kiasi cha Tsh Millioni 23 zimeshatumika, na majengo hayo yanatarajia kugharimu kiasi cha Tsh million 32,843,000/=
Ziara ya Mkurugenzi hiyo iliendelea hadi katika Shule ya Sekondari Lubengera awali iliyokuwa Shule ya Msingi Kigoma ili kukagua ukarabati unaoendelea , akipewa taarifa na Mkandarasi wa kazi hiyo alisema hadi sasa kazi hiyo ya ukarabati wa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 70, huku kazi kubwa iliyosalia ikiwa ni kazi ya upakaji rangi kwa nje na ujenzi wa ukuta wa kutenganisha shule ya msingi Kigoma na Shule hiyo ya Sekondari
Aidha ziara iliyofanyika hadi katika ujenzi wa chumba kimoja katika shule ya Msingi Benjamini ambapo Mkurugenzi alipewa taarifa na mwalimu Mkuu wa shule hiyo Ndugu. Runuguye Kalabona kuwa ujenzi wa darasa moja umefikia hatua ya upauaji huku kiasi cha Tsh million 10, zikiwa zimetumika katika ukamilishaji wa boma, huku akimuomba Mkurugenzi huyo kuleta fedha nyingine za umaliziaji wa jengo hilo
Mwalimu mkuu huyo alimpongeza Mkurugenzi huyo na Kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kuleta fedha za ujenzi, huku akisema tayari Serikali Kuu imeleta kiasi cha fedha million ishirini na tano(25,000,000/=) ili kuanza kujenga nyumba za walimu wa shule hiyo
Mwalimu mkuu huyo alihitimisha kwa kueleza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kutokana na wingi wa wanafunzi wa shule hiyo kuwa wanafunzi 1369 na kuwa na vyumba vya madarasa 9 hali inayoweza kuzolotesha suala la ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi
Mkurugenzi huyo alihitimisha ziara katika kukagua ujenzi wa ofisi ya kata ya Bangwe, akiwa katika eneo hilo Mtendaji wa Kata hiyo Ndugu . Kalukura alisema ujenzi umefikia asilimia 85, na mafundi wako hatua ya upakaji rangi na jengo linatarajia kukamilika hivi karibuni na kiasi cha fedha Tsh Million 35 zinataria kukamilisha ujenzi wa Ofisi hiyo, na kiasi kilichotolewa na Serikali Kuu ikiwa ni Kiasi cha shilingi million 31, huku Mkurugenzi akiahidi kutoa kiasi cha shilingi Millioni 4 ili kukamilisha ujenzi huo
Akiwa katika ziara hiyo Mkurugenzi alisema “Halmashauri imezamilia kukamilisha miradi viporo ndio maana tumeanza na viporo vya ujenzi wa nyumba mbili za walimu shule ya Msingi Ujiji na ujenzi wa Zahanati eneo la Buronge, Na mimi na watendaji wangu wananipa ushirikiano katika kuhakikisha tunasimamia ujenzi wa miradi hii ili kuwa katika ubora unaohitajika”
Hata hivyo Mkurugenzi huyo aliahidi kukarabati madarasa chakavu katika shule ya Msingi Ujiji huku akiridhishwa na kasi ya ukarabati inayoendelea katika Sekondari ya Lubengera na kuahidi kuendelea kuongeza vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Benjamini.
PICHA ZA ZIARA NZIMA INGIA KATIKA MAKTABA YA PICHA KATIKA TOVUTI YA www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa